Mratibu wa kituo cha jimolojia Tanzania Bw.Musa Shanyangi akiongea na waandishi wa habari hivikaribuni kuhusu namna kituo hicho kinavyotoa mafunzo ya ukataji madini ya vito
Mwalimu msaidizi wa chuo hicho Bw.Jamal Dallos akiwa anaendelea na shughuli ya ukataji madini
Lilian Petro akikata madini kwaajili ya kutengeneza pete,mkufu ,jiwe hilo ni aina ya Quartz shape Oval
Grace Charles akiendelea na ukataji wa madini
Kulia ni Gladness John pamoja na Loveness Marteen wakiwa wanaendelea na shughuli ya ukataji
Magret Joseph akiwa anaangalia kwa makini namna alivyokuwa akikata jiwe kwa kutumia mashine maalum
Loveness
Marteen anachukua fursa hiyo kuwataka wanawake wengine kujitokeza
katika fani hiyo ya ukataji madini kwa kuwa hata wanawake wanaweza
kufanya shughuli hizo kama wanaume
Aina mbalimbali ya madini kabla ya kukatwa
Baada ya kukatwa na mashine muonekano huwa hivi
Wanafunzi wakiwa darasani wakiwa wanaendelea na shughuli ya ukataji madini
Sekta ya madini nchini bado inakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo uhaba wa walimu na wataalamu wa kufundisha ukataji wa
vito vya madini hali inayosababisha kuuzwa kwa madini ghafi nje ya nchi
na kupelekea kuuzwa kwa bei ya chini na pesa nyingi kwenda nje
Hayo yameelezwa leo na mratibu wa kituo cha jimolojia Tanzania Bw.Musa
Shanyangi wakati akiongea na waandishi wa habari katika kituo hicho
kina kinachotoa mafunzo ya ukataji madini ya vito wakati wa mahojiano
maalum na waandishi wahabari chuoni hapo ambapo wameanza kutoa mafunzo
ngazi ya cheti kwa wahitimu 15 wakike ambapo chuo kipo katika
halmashauri ya manispaa ya jiji la arusha.
Alieleza kuwa hivi sasa madini ghafi yanauzwa sana nje ya
nchi kwa bei ya chini lakini kama wangeweza kuuza madini hayo yakiwa
yameongezwa thaman na kuuzwa kwa bei ghali na kuwezesha fedha za kigen
kubaki nchini na kuongeza pato la taifa .
Bw,Shanyangi aliongeza kuwa hivi sasa wameanza kuwafundisha
kozi ya miezi 6 kwa wanafunzi 15 wakike ambapo wanafadhiliwa na Arusha
women foundation fund iliyoko mjini ikiwa na lengo la kuwasaidia mabinti
ili kuweza kusaidia sekta ya madini na kuweza kukabiliana na uhaba wa
wataalamu wa ukataji madini nchini.
Hata hivyo kituo hicho kinatarajia kuongeza wanafunzi mpaka
kufikia 60 ili kuweza kuongeza ufanisi na kuweza kuboresha sekta hiyo ya
madini ili kuweza kuongeza wataalamu ,pia wanamkakati wa kuweza
kusomesha walimu wazawa ili kuweza kukidhi nakuwa na walimu na kupunguza
gharama za kuchukua mwalimu kutoka nje yanchi ambapo hivi sasa
wamemuajiri raia kutoka Sri lanka hali ambayo wanatumia gharama kubwa
kumlipa mtaalamu huyo toka nje ya nchi.
BwShanyangi aliwataka wadaumbalimbali nchini pamoja na
wawekezaji wawekeze katikak kufundisha wataalamu wazawa ili kuweza
kukidhi mahitaji ya wakataji na wataalamu nchini.
Kituo hicho kimegharimu zaidi ya shilingi billion 1.2na
mashine mbalimbali za kituoni hapo zimegharimu zaidi ya milioni 450 za
ukataji na kusafisha madini hayo
Kwa upande wake mwanafunzi katika chuo hicho Bi.Joice
Patrick alisema kuwa kupitia mafunzo hayo ya ukataji wa madini na
ung’arishaji itawasaidia katika swala zima la ajira huku akiwataka
wanawake kuchangamkia fursa hiyo
“Ni fursa sasa kwa wanawake kujitokeza katika kazi hii na waione kama kazi zingine na si kuwaachia wanaume tu “alisema Joice