JAJI AUGUSTINO RAMADHANI AKUTANA NA MWAKILISHI WA "FRANCOPHONIE" ARUSHA LEO
Posted by
woinde
on
Monday, February 23, 2015
in
Habari
MATUKIO
|
|
Rais
wa
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu(AfCHPR)Jaji Augustino
Ramadhani(kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Naibu
Mwakilishi Mkazi wa taasisi ya kimataifa
“La Francophonie” katika Umoja wa Afrika(AU)yenye makao yake Addis
Ababa,Ethiopia,Cecile Folchini kwenye ofisi za Mahakama ya Afrika
jijini Arusha leo. |
|
Rais
wa
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu(AfCHPR)Jaji Augustino
Ramadhani(wa pili kulia)akiwa katika picha ya pamoja na Naibu
Mwakilishi Mkazi wa taasisi ya kimataifa
“La Francophonie” katika Umoja wa Afrika(AU)yenye makao yake Addis
Ababa,Ethiopia,Cecile Leque Folchini(kulia)kushoto ni Msajili wa
mahakama hiyo,Dk Eno Robert na Mkurugenzi wa Alliance Francaise
d'Arusha,Gaelle Lapostolle.
Mwandishi Wetu
Rais
wa
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu(AfCHPR)Jaji Augustino
Ramadhani leo amefanya mazungumzo na Naibu
Mwakilishi Mkazi wa taasisi ya kimataifa
ya “La Francophonie” katika Umoja wa Afrika(AU)yenye makao yake Addis
Ababa,Ethiopia,Cecile Folchini kwenye ofisi za Mahakama ya Afrika
jijini Arusha ambayo yamejikita kushirikiana baina ya taasisi hizo mbili.
Cecile
alisema taasisi yake iko mbioni kuona ni namna gani wataisaidia
Mahakama hiyo ya Afrika ya Haki za Binadamu ili kuiwezesha kufanya kazi
zake ipasavyo.
Katika
ujumbe wake aliambatana na Mkurugenzi wa Alliance Francaise
d'Arusha,Gaelle Lapostolle ambayo hutoa mafunzo ya kifaransa ambayo
iliahidi kutoa mafunzo kwa Majaji wa Mahakama hiyo kujifunza kifaransa
katika muda wao wa ziada.
Mahakama
hiyo ina Majaji kutoka nchi mbalimbali zikiwemo zisizotumia lugha ya
kifaransa kama lugha rasmi zikiwemo Afrika Kusini,Tanzania,Uganda,Malawi
na Kenya.
Lugha rasmi za Mahakama hiyo ni Kiingereza,Kifaransa,Kireno na Kiarabu. |
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia