Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua akijadiliana jambo na Viongozi wa
Kamati ya Shule ya msingi Kulala mara baada ya kukabidhi mifuko 50 ya
saruji ikiwa ni mchango wa Mbunge huyo katika kusaidia ukarabati wa
shule hiyo.Jumla ya shule tatu za msingi Sura,Kulala na Ulonga
zilikabdidhiwa mifuko 150 ya Saruji
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari akisomewa kitabu cha Hadithi
na Mwanafunzi wa shule ya Msingi Sura iliyopo wilaya ya Arumeru jana
alipofika kutoa mchango wa mifuko 50 ya saruji katika kusaidia ukarabati
wa
shule hiyo.Jumla ya shule tatu za msingi Sura,Kulala na Ulonga
zilikabdidhiwa mifuko 150 ya Saruji
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari akisomewa kitabu cha Hadithi
na Mwanafunzi wa shule ya Msingi Sura iliyopo wilaya ya Arumeru jana
alipofika kutoa mchango wa mifuko 50 ya saruji katika kusaidia ukarabati
wa
shule hiyo.Jumla ya shule tatu za msingi Sura,Kulala na Ulonga
zilikabdidhiwa mifuko 150 ya Saruji
Shule za Msingi za Sura, Kulala na Ulonga zilizopo wilaya ya
Arumeru zinakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa majengo pamoja na ukosefu wa
huduma za choo hali inayoathiri hali taaluma katika shule hizo.
Akizungumzia changamoto hizo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi
Sura Sifaeli Akiyoo amesema kuwa hali ya Taaluma shuleni hapo
itaboreshwa iwapo kutakuwepo na mazingira mazuri ya Wanafunzi kujifunzia wawapo
shuleni hivyo ameiomba jamii kujitokeza kusaidia shule hiyo ili iweze kufanya
vizuri kitaaluma.
Mtendaji wa Kijiji cha Sura Kaanael Pallangyo amesema kuwa juhudi
za wananchi na mashirika pamoja na serikali zinahitajika ili kuwajengea
wanafunzi mazingira bora ya kujifunzia na ili waweze kufaulu vizuri katika
masomo yao.
Kutokana na Changamoto hiyo Mbunge wa Arumeru Mashariki
Joshua Nassari ambapo amechangia mifuko 150 ya saruji katika shule za Sura,
Kulala na Ulonga ili kuwezesha ukarabati wa majengo ya shule hizo ambazo hali
yake bado hairidhishi.
Nassari amewaasa Wananchi wa vijiji hivyo kuunganisha nguvu
na kushirikiana na serikali ya Kijiji
katika kuboresha hali ya elimu .
Sekta ya Elimu ni sekta nyeti nchini ambayo ikitiliwa mkazo
inaweza kusaidia kupunguza umasikini,maradhi na ujinga ,hivyo jitihada za dhati
zinahitajika ili kuifanya elimu kuwa silaha bora itakayowasaidia Vijana na
Watanzania kubadilisha maisha yao na kuliletea maendeleo taifa.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia