Kituo cha
kukuza soka la vijana cha Future Stars Academy(FSA) cha jijini Arusha kinataraji kushiriki katika michuano ya Uganda Junior League inayotaraji
kutimua vumbi jijini Kampala mnamo Aprili 24 hadi 26 mwaka huu.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi na mwanzilishi wa kituo hicho,Alfred Itaeli alisema kuwa kituo chao kinataraji
kupeleka timu ya watoto ya U-15 katika michuano hiyo kwa lengo la kushindana na kisha kunyakua ubingwa.
Alisema
kuwa ushiriki wao umefuatia kupitia
mwaliko walioupata kutoka nchini Uganda kutokana na nchi hiyo kutambua jitihada za kituo chao za kukuza soka la
vijana hapa nchini pamoja na ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hatahivyo,mkurugenzi
huyo alisisitiza ya kwamba katika kuhakikisha wanashriki mashindano hayo kituo
chao kimeanza mkakati wa kusaka fedha za nauli na matumizi wakiwa nchini wakati
wote wa mashindano kwa kusaka udhamini kutoka kwa wadu mbalimbali wa soka mkoani Arusha na nchini kwa ujumla.
Alisema kuwa
wameanzisha tamasha la soka liitwalo “Quiz Night” ambalo linataraji kufanyika
mnamo febuari 28 mwaka huu katika viwanja vya TGT jijini Arusha ambapo
wanataraji kukusanya fedha za ushiriki katika tamasha hilo ili ziweze
kuwasaidia katika safari yao nchini Uganda.
Itaeli,aliwataka
wadau mbalimbali wa soka mkoani Arusha ana nchini kwa ujumla kuwapa sapoti
katika safari yao kwa kuwa hadi sasa wamekusanya kiasi cha sh,2 milioni ambapo kwa safari yote nchini humo
kinahitajika kiasi cha sh,7 milioni.
HABARI kwahisani ya libeneke la kaskazini blog
HABARI kwahisani ya libeneke la kaskazini blog