PRODUCER WA XO YA JOH MAKINI “SAPPY” AFUNGUKA USIYOYAJUA KUHUSU WEUSI
Huyu
ni kijana wa Kitanzania ambaye amejipatia Umaarufu wa Kupika Midundo ya
Tofauti sana ya Muziki hapa Afrika Mashariki. Sappy amefanya kazi na
Wasanii Kibao hadi sasa Kama Prezzo ambaye alimuundia ngoma ya Marry
Marry na My Girl, Kafanya Kazi na Kaka Sungura Rabbit, Nazizi na Wasanii
wengine Kibao wa Kenya.
Heshima
Kubwa sana aliipata kupitia ngoma ya Budder than Most ya Redsun ambayo
Remix yake alishirikishwa Mkali Demarco toka Jamaica na sasa Heshima ya
Sappy kwa Tanzania imeongezwa na XO Ngoma kali toka kwa joh Makini
akishirikishwa Baba Samantha GNako.
- JOH MAKINI & pRODUCER SAPPY
Akiongea na @DJHAAZU ndani ya Kipindi cha Dundo cha Mambo Jambo Radio Mapema
Leo Sappy ameelezea Historia yake hadi kuja Kufanya kazi na Weusi
wasanii ambao anasema Alikuwa na ndoto ya kufanya nao Kazi toka kitambo
sana.
Sappy
alienda Kenya Kusomea Muziki akiaamini kuwa Muziki unahitaji Elimu
zaidi ya ambavyo watu wanafikiria na Alivyoenda Kenya Kusoma akagundua
kuwa Muziki Unavyofanywa Kenya unafanywa Kisomi Zaidi tofauti na
Tanzania.
Katika
Mazungumzo yake akatiririka Mengi haswa alivyokuwa akitamani Siku moja
afanye Kazi na Vijana ambao anaamini Wanajitambua na wanajua
wanachokifanya WEUSI
NAZIZI & SAPPY
PATA NAFASI YA KUMSIKILIZA KWA KU-CLICK LINK HII HAPA:- PRODUCER SAPPY KENYA KUNA KITABU CHA MUZIKI ....BY @DJHAAZU
Endelea
Kusikiliza Dundo la Mambo Jambo Radio 93.0 FM na Dj Haazu na pia
Endelea kufuatilia hapa Kujua Mengine aliyoyaongea Producer Sappy
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia