Nimefikia
uamuzi wa kudai talaka kutokana na kuchoshwa na vitendo vya ukatili
nilivyokuwa nafanyiwa na mume wangu, kwa zaidi ya miaka8 na hata sasa
bado anaendeleaje, Kwani hata kuongea uongo kwenye media juu yangu ni
ukatili pia.. nimekuwa nikinyanyaswa kijinsia na
mume wangu na sikuwahi kutoa taarifa mahala popote kutokana na vitisho alivyokuwa akinitisha.
Watu
Wengi wanafikiri nilikuwa na ndoa nzuri sana lakini kumbe nilikuwa
Nikivumilia tu Kwani niliamini ipo siku atabadilika maana nilimpenda
sana mume wangu.Nilijaribu kuficha huzuni na maumivu yangu kila
nilipotoka na mume wangu kwenda kwenye Huduma au mahala pengine penye
mkusanyiko wa watu.
Sijawahi
hata Mara moja kutoa taarifa hata kwa wazazi wangu juu ukatili
niliokuwa nafanyiwa na mume wangu.Kwanza sikutaka kumvunjia heshima kwa
ndugu zangu na pia alikuwa akinitishia kuniua na kuongeza kunifanyia
ukatili huo.
Kutokana na historia yake ya nyuma alikuwa na uwezo wa kunifanya chochote na ndiyo maana nilikuwa nikimwogopa sana.
Siku
zote nilikuwa akilala na panga kitandani ambalo ndilo alikuwa akinipiga
nalo na kuapa kunichana chana Mwili Kabla ya kuniua.
Kipigo
hicho nimekuwa nikikipata hata ninapokuwa kwenye Huduma bila kujali
natakiwa kuwa kwenye mood nzuri ili ni perfome vizuri.
Nimevumilia
muda mrefu lakini ndo mateso yakawa yanazidi na kufikia hatua ya
kufukuzwa akidai yeye ana mwanamke mwingine wa dini yake ya zamani hivyo
anataka amlete hapo nyumbani.
Nilikataa
kuondoka na kumwambia amlete tu, tutaishi wote mimi nitakuwa nikilala
chini maana nshazoea siku zote Amekuwa akinilaza chini ,alivyoona siku
zinazidi kwenda na mimi nimegoma kuondoka basi akaamua sasa isiwe siri
ya chumbani tena Akawa ananitoa ananipigia sebuleni na anasema nataka
mtoto na wengine wote wajue kuwa huwa nakupiga humu ndani.Ikafika hatua
anataka kunitoa nje ya geti ili majirani wajue kuwa huwa napigwa na
anifukuze mbele yao.
Kwa
Miaka yote alinizuia kufungua account bank na kudai kuwa yeye ndo
mwanaume hivyo pesa zote ataweka yeye. So pesa zangu zote nilizokuwa
naingiza alikuwa akichukuwa yeye na kuzihifadhi kwa account yake
binafsi.
Sikuwa
nikibaki hata na mia.Nilijaribu kufanya biashara lakini napo pesa zote
akawa akichukuwa yeye ikabidi niache.. Nikitaka hata vocha ya mia tano
Lazima nimwombe hela na niitolee maelezo ninampigia nani.
Mume
wangu kwa kipindi chote hakuwahi kuwa na kazi yoyote zaidi ya kunifanya
mimi ndo biashara yake. Lengo lake ilikuwa ni kunitumia mimi kwa
maslahi yake na sio upendo kama mke wake.
Hakuwahi
kunipenda hata yeye mwenyewe hukiri kuwa alinioa tu basi ili afanikiwe
kwenda ulaya kwa kuwa mimi nilikuwa nikisafiri na babu yangu.
Na
yeye kila akijaribu kwenda nje anashindwa. Kuna mambo mengi ya ukatili
aliyokuwa akiyafanya ndani siwezi kuyasema kwa ajili ya maadili na pia
bado Ninamheshimu kama mzazi mwenzangu. Alipoona siondoki pamoja na
vipigo, matusi na kunifukuza kote.
Akasema
nitahakikisha nakufanyia jambo ambalo utaondoka mwenyewe humu ndani
bila kupenda sitaki kuzungumzia suala ambalo liko mahakani ingawa hilo
nahisindilo alilokuwa kadhamiria ili tu niondoke.
Nilijaribu
sana kumsihi tukae kikao na wazee ili watushauri na kutusaidia lakini
nilikuwa nikiambulia matusi tu ya nguoni ambayo siwezi kuyaandika hapa.
Siku
niliyoondoka nyumbani alidhamiria kuniua alidai hata akiniuà hakuna
atakaye amini kuwa ni yeye kaniua, na ni kweli maana sikuwahi kushtaki
mahala popote.
Alichukuwa
panga akanipiga nalo kisha akaniniga hadi nikaishiwa nguvu
.Aliponiachia sielewi nilitokaje ndani. Ugomvi mkubwa ulitokana na mimi
kukataa kufanya tenda la ndoa kinyume na maumbile.
Amekuwa
Alinipiga na kunilazimisha kufanya tenda hilo kinyume na maumbike kwa
miaka mingi lakini nikisema bora nife kuliko kutendewa ukatili
huo.Amekuwa akidai kuwa wanawake tumeumbwa ili tufanyiwe tenda hilo la
ndoa mbele na nyuma so ni haki yake.
Niliondoka
kwake nikiwa na sh elfu mbili tu. Nilimwachia kila kitu nyumba gari na
pesa zote zikiwa kwa account yake zaidi ya milioni 50.Sikuwa na uwezo wa
kutoa pesa maana ni account yake binafsi.
Nimejitahidi
sana kumwita kwenye vikao hata vya familia ili tu tujaribu kuzungum za
lakini amekuwa akionesha dharau tu na kusema yeye haitaji ndoa tena
anaoa mke mwingine hivyo hawezi kusuluhishwa.
Ingawa Amekuwa akidanganya sana kwenye media. Nilimwuliza Unapata faida gani unapodanganya watu kuhusu mimi?
Akasema
yeye amechafuka kwa ubakaji so acha na mimi nichafuke na akasema
atahakikisha sifanyi huduma sehemu yoyote labda nihame nchi.
Kama
msg hizo angekuwa amezituma bila kuandika na matusi ningezikopi but
zaidi kauli zake ni za matusi. Hivyo imefika mahali nimeona bora
tuachane kisheria na pia nipate haki yangu maana mume wangu anajivunia
mali ambazo hakuzitolea jasho yeye na huku anawatapeli watu kwa kudai
kuwa hana pesa maana mimi nimeondoka nazo wakati ni uongo mtupu.
Mimi
ninapanda daladala siku hizi sababu sina uwezo wa kuwa na gari hadi
niazime kwa marafiki zangu. Mume wangu amekataa hata kumsomesha mtoto
sasa hivi nahangaika kutafuta ada ili mtoto arudi shule lakini pesa yote
anayo Mbasha.
Sasa
sijui hapo ananikomesha mimi au mwanaye.!maana urithi wa mtoto ni elimu
bora na mzazi anayempenda mwanaye atapambana ili kuhakikisha mtoto
anapata elimu bora.
Nilikaa
kimya muda mrefu sikutaka kuzungumza lakini imefika mahali Nimechoka
maana huyu bwana hajiheshimu. Tukikutana anasema sio yeye anayepeleka
habari mitandaoni.
Ninaomba
wanaume wenyewe Mfano wake waache kuwafanyia ukatili wake zao
majumbani.Najua wako Wengi sana wanao nyanyasika kama ilivyo kuwa kwangu
lakini Hawana sehemu za kukimbilia Hivyo wanavumilia tu na mwisho wa
siku wanakufa na kuacha watoto wakiteseka.
Mimi
Nilivumilia zaidi ya Miaka 8 lakini imefika mahali enough is enough.
Maandiko matakatifu yanasema, ndoa haivunjwi isipokuwa kwa uasherati.
Acha nife kwa mapenzi ya Mungu na sio kwa mapenzi ya mtu..Na ni naamini sitakufa mpaka ndoto zangu zitimie.
Mume
wangu ameapa kuwa atahakikisha sifanyi Huduma tena lakini ninasema
katika Jina la YESU, kama Bwana aishivyo, mwanzilishi wa huduma yangu ni
Mungu Hivyo mmalizaji wa Huduma yangu ni Mungu mwenyewe.
Na
sasa ninajipanga kumwimbia Mungu kama sitaimba tena.Wakati mwingine
usipokuwa mwangalifu ndoa inaweza kukukosesha ufalme wa mbinguni hasa
Ukiingia kwenye ndoa isiyo sahihi. Ninampenda sana mume wangu lakini
ninampenda Mungu wangu zaidi. Ahsante.
Nimeamua
kuandika Maana Nimechoka kuficha maovu aliyokuwa
akinitendea.Nimemtunzia heshima muda wote maana sikutaka jamii imjue ni
mtu wa aina gani but yeye anatumia ukimya wangu kama udhaifu so naona
bora niweze wazi ili jamii imtambue mimi yamenikuta najua Wapo Wengi tu
wanapitia mateso niliyoyapitia mimi.
Kutokana
na vitisho wanaendelea kunyanyaswa. That is not fair kwa kweli.Mimi
ningekufa Kabla ya wakati wangu lakini namshukuru Mungu niko hao hata
sasa na pia ili kuwaonya wanaume wanaume wenyewe tabia kama yake.
Kama umemshoka mwanamke achaneni kwa amani sio kumnyanyasa mwanamke kama alivyokuwa anafanya Mbasha kwangu.
Ninapinga vikali unyanyasaji wa wanawake na watoto majumbani