Mbio
za 13 za Kilimanjaro Marathon ambazo zimepangwa kufanyika Machi 1, 2014
mjini Moshi mkoani Kilimanjaro zimepata msisimko mpya baada ya
wanariadha nyota wa Tanzania kuthibitisha kushiriki.
Mkurugenzi
wa Mbio hizo John Bayo jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari
aliwataja baadhi ya wanariadha nyota kutoka Tanzania kuwa ni Andrew
Sambu, Daudi Joseph, Mashaka Masumbuko, watachuana na wanariadha wengine
kutoka nchini na kutoka nje ya nchi katika mbio za Kilimanjaro Premium
Lager Marathon kwa wanaume za kilometa 42.195.
Kwenye
upande wa marathon wanawake Fabiolla William, Sarah Maja and Banuelia
Katesigwa ni miongoni mwa nyota wa Tanzania watakaochuana na wenzao
kutoka ndani na nje ya nchi katika kuwania tuzo mbalimbali kwenye Mbio
za Kilimanjaro Premium Lager Marathon kwa wanawake za Kilometa 42.195.
Aidha,
wanariadha Fabian Fabian Joseph, Alphonce Felix, Dickson Marwa
wamethibitisha kushiriki Tigo Kili Half Marathon wanaume wakati Mary
Naali, Natalia Elisante, Catherine Lange na Jacqueline Sakilu ni
miongoni mwa majina maarufu katika riadha yaliyothibitisha kushiriki
kupitia kundi la wanawake litakalochuana katika Mbio za Tigo Kili Half
Marathon.
Katika
mbio za nusu marathon ambazo Tanzania ina historia ya kufanya vizuri,
Fabian Joseph ana rekodi ya ushinda Kilimajaro Marathon mwaka 2010
ambapo alimaliza mbio katika muda wa 1:3;59 na vilevile ana rekodi ya
kushinda Edmonton Marathon mwaka 2005 kwa muda wa 1:01:08.
Akiwa
ametengeneza rekodi nyingi, Mary Naali ni kati ya wanariadha bora nchini
katika mbio za kilomita 21 maarufu kama Half Marathon. Alishinda Vienna
Marathon mwaka 2010 ambapo alimaliza katika muda wa 1:12:16 na baada ya
hapo akavunja rekodi kwenye mbio za kilomita 25 za Arusha VIP Race
mwaka 2011 ambapo alishinda kwa 1 1:20:52 na kuvunja rekodi ya 1:22:18
iliyokuwa imewekwa na Josephine Deemay mwaka 2006. Mei mwaka 2013 pia
alishinda mbio ya Bucharest International Marathonihuko Romania
akimaliza katika muda wa 1:16:32.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia