Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez (katikati) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie
Manento (kushoto) wakitiliana saini makubaliano ya ushirikiano wa
kukabiliana na ugonjwa wa ebola kwa kutoa elimu kwa jamii kupitia ujumbe
mfupi maneno katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za Mratibu mkazi
wa mashirika ya Umoja wa Mataifa jijini Dar. Anayeshuhudia tukio hilo ni
Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dkt. Jama Gulaid.(Picha na Umoja wa
Mataifa).
Na
Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya simu ya Push Mobile imetiliana saini na
serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa (UN) ya kuwafikia watu milioni 10
ikiwahabarisha kuhusu ugonjwa hatari wa ebola.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa mjini hapa kampuni hiyo
ya simu imesema kupitia ushirikiano huo kampuni hiyo ya simu itaunga mkono
juhudi za serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa wa kutoa elimu dhidi ya
ugonjwa huo ujumbe mfupi utakaoelezea ugonjwa wa ebola.
Kama
sehemu ya makubaliano, Push Mobile , UN, serikali na wadau wake watatoa
taarifa kuhusu ugonjwa huo wanapohitajika.
Watanzania wanaweza kupata habari za ugonjwa huo kwa
kuandika neno EBOLA kwenye namba 15774 na kupata taarifa za ugonjwa huo
bure bila kutozwa gharama.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento
wakionyesha hati za makubaliano ya ushirikiano huo.
Wakitia saini Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie
Manento amesema kwamba kama Ujumbe mfupi unaweza kuokoa maisha kampuni yake
iko tayari kushiriki katika kampeni hiyo.
"..Teknolojia inatoa fursa ya pekee ya kuandaa jamii
dhidi ya ugonjwa wa ebola na nini cha kufanya ukitokea. Kupitia ushirikiano
huo kati yetu na Umoja wa Mataifa na Wizara ya afya na ustawi wa jamii
tunaamini tutasaidia wananchi kuelekewa na kutambua dalili za ebola, kuzuia
na kudhibiti maambukzi ya virusi vya ebola", alisema
Manento.
Katika
miezi iliyopita vifo kutokana na ugonjwa wa ebola vimefikia 9000 huku vifo
vingi vikitokea katika nchi za Liberia, Sierra Leone, na Guinea. Hadi sasa
watu 23,000 wameelezwa kukumbwa na ugonjwa.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento kwa
pamoja wakionyesha ujumbe mfupi wa maneno unaotoa elimu ya ugonjwa wa ebola
kwa baadhi ya wageni waalikwa na waandishi wa habari (hawapo pichani)
waliohudhuria hafla hiyo.
Tanzania ikiwa na watumiaji wa simu milioni 30 na kufanya
uwezekano wa kufikia watu hao kuwa ni asilimia 68.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro
Rodriguez amesema teknolojia ya simu itasaidia sana kuleta uelewaq wa
ugonjwa huo miongoni mwa Watanzania.
"Mlipuko wa ugonjwa wa ebola umepungua sana Afrika magharibi na Tanzania
haijawahi kukumbwa na ugonjwa huo.
Lakini kunahitajika mtu mmoja tu kuwa na ugonjwa huo na kuleta mashaka
makubwa katika maisha ya watu nchini. Tukiungana na sekta binafsi, Umoja wa
mataifa unaunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania kupitia wizara ya afya
na ustawi wa jamii kuongeza upeo wa utayari katika kukabiliana na Ebola
."
Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dkt. Jama Gulaid
akimshukuru Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento (kushoto)
mara baada ya hafla fupi ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano huo.
Kulia ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akishuhudia tukio hilo.