Simu ya Obi aina ya
S550-Crane.
Na
Mwandishi Wetu
MWANZILISHI mwenza wa kampuni ya kimataifa ya teknolojia
ya mawasiliano ya Obi Mobiles, yenye makao makuu yake Singapore, John
Sculley amesema ujio wa kampuni hiyo nchini Tanzania, utaongeza wigo wa
utumiaji wa tehama na hasa matumizi ya zana za kisasa za
mawasiliano.
Obi
Mobile inatumia teknolojia iliyobuniwa mjini Toronto, Canada na kampuni ya
Inflexionpoint.
John
Sculley, ambaye alishawahi kuwa ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Apple
amesema teknolojia hiyo mpya ambayo ilizinduliwa India na Mashariki ya Kati
mwaka 2014 imelenga kuwanufaisha vijana ambao ndio watumiaji wa kubwa wa
simu za kisasa.
Amesema kwa kuingiza bidhaa za Obi nchini Tanzania
wanatarajia kuwawezesha vijana kuwa na simu ambazo zinawatumikia wao kwa
maarifa na umaridadi zaidi.
S550-Hornbill.
"Simu
hizi zimepokewa vyema zilikozinduliwa na tunararajia Tanzania nazo
watazipokea kwa kasi hiyo hiyo" alisema Sculley .
Kwa
mujibu wa ofisa huyo, simu za Mobile nchini Tanzania zinauzwa kati ya sh
50,000 na bei ya juu ni 350,000.
Alizitaja aina hizo za simu kuwa ni Hornbill S551;
Falcon S451; Crane S550; Wolverine S501; Fox S453 ; Racoon S401 na Power
GO F240 simu ambayo ina betri yenye uwezo wa 2,800mAH na yenye uwezo wa
kuchaji simu nyingine.
Amesema watu wa Obi Mobiles wanaamini kwamba teknolojia
ni kwa ajili ya watu wote na ndio maana mauzo ya teknolojia zao ni rahisi
kwa ajili ya watu wote.
Alisema kwa kuwa na vifaa vya teknolojia ya Obi, vijana
watakuwa na nafasi ya kutumia fursa zilizopo za kiuchumi na
kijamii.
S453-Fox
Sculley amesema kwa muono wake teknolojia haitakiwi kuwa
ngumu kuitumia wala kutengeneza changamoto kwa watumiaji wake kwa kuiwekea
vikwazo.
Teknolojia za Obi Mobile zinazotumia mfumo wa Android ni
za daraja la juu na wkamba simu zote za Obi zilizoingizwa nchini zina uwezo
wa kuwa na intaneti.
Kampuni hiyo inatarajia kuzindua simu hizo nchini
Tanzania mwezi ujao .
Akizungumzia mkakati wa kampuni hiyo kwa bara la Afrika
, Mkurugenzi Mtendaji wa Obi Mobile MENA, Amit Rupchandani: "Walaji wengi
wanataka kujiondoa katika simu za kawaida kwenda katika simu za kisasa.
Hata hivyo,gharama za uwekezaji katika teknolojia ya kisasa ni kikwazo
kikubwa kwa watu wengi."
Obi
Mobiles, wamesema kwamba kwa kuelewa hilo, wamewezesha kuwa na simu zenye
uwezo mkubwa na kwa bei nafuu ili kufikia kila kundi katika bara la
Afrika.
Simu
hizi ambazo vijana watazipenda zimeelezwa kutengenezwa kumudu maisha yao na
kuwapendezesha.