Mwenyekiti
wa Chadema Taifa Mhe Freeman A.Mbowe akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa
Kanda ya Kaskazini Mhe Israel Natse wakiwa wanaingia ukumbi wa JUMUIKA
Viongozi wa kuu wa Chadema Taifa pamoja na Kanda wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kikao cha baraza la kanda ya kaskazini kuanza
Waheshimiwa wabunge wakiwa wanaimba wimbo wa Taifa
Katibu
wa Kanda ya kaskazini Mhe Amani Golugwa akiwakaribisha wajumbe wa kikao
cha baraza la Kanda ya Kaskazini , wajumbe wa kikao wametoka katika
majimbo 33 ya kanda
Mwenyekiti wa Kanda ya kaskazini Mhe Israel Nates akitoa neno la ufunguzi kwa wajumbe na kumkaribisha Naibu katibu Mkuu Zanzibar
Naibu
katibu Mkuu Zanzibar Mhe Salimu Mwalimu akiongea na Wajumbe wa baraza
la uongozi wa kanda ,na kufafanua majukumu na utekelezaji wa kanda
kaitika ujenzi wa chama
Mhe
Freeman A.Mbowe akiwa hutubia wajumbe wa baraza la kanda pamoja na
waandishi wa habari, akifafanua baadhi ya mambo ambayo yanaendendea
katika nchi yetu kwa sasa, pia akiitaka tume kuwa na msimamo wa siku na
tarehe ya kuanza zoezi la uandikishaji wa Wanachi kwenye daftari la
kupiga kura
Mwenyekiti huyo amesema kuwa chama
chao kimejipanga kuahakikisha kinahamasisha kwa nguvu zote wananchi
weweze kwenda kujiandikisha katika daftari la mpiga kura
Alisemakuwa
hii itaweza kumsaidia kila mwananchi kuweza kupata haki yakumchagua
kiongozi bora anaemtaka katika uchaguzi mkuu ujao wa kuwachagua
viongozi wakuu ambao ni rais ,wabunge na madiwani.
Alisema
kuwa pamoja ya kuwa tume wamekuwa wananchelewesha kufanyika kwa zoezi
hili , wao wamejipanga kikamilifu na pindi ambapo zoezi hili
litatangazwa kuanza rasmi watajitaidi kwa njia yoyote kuhamasisha
wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha
Alisema kuwa kwa
upande wa kupiga kura katiba wanaendelea na msimamo wao ambao
walitangaza awali wa kutoshiriki katika mchakato wa kura ya maoni ya
katiba huku akisisitiza kuwa swala la kutoshiriki katika mchakato
wakura za maoni auingiliani kabisa na kuhamasisha wananchi
kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura
Alimaliizia
kwa kuwasihi wananchi wajitokeze kwa wingi sana pindi pale ambapo
watasikia zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu limewadia ili
waweze kupata haki yao ambayo itawaruhusu kuchgua kiongozi wanao
wataka.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia