Wanachama wa C hama cha Mapinduzi wametakiwa kushirikiana na kuvunja
makundi ili kuleta umoja na mshikamano utakaokisaidia chama hicho
kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu kama ilivyokuwa kwenye uchaguzi wa
serikali za mitaa.
Kauli hiyo imetolewa na
Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Arusha mjini Dkt. Willfred ole
Soiley wakati wa mkutano wa kuwashukuru Wananchi kwa kukipa chama hicho
mitaa yote ya Kata ya Kaloleni kwenye viwanja vya ofisi ya Mtendaji wa
kata hiyo.
Alisema kuwa kushindwa kwa chama
hicho kunatokana na wanachama kuendekeza makundi yasio na lazima kwa
mwenye kupata ridhaa ni mmoja hivyo wote kumuunga mkono alieshinda na
hivyo kukiwezesha chama kupata ushindi na si vingine.
Dkt. Soiley alisema kuwa
wanachama wa chama hicho wanatakiwa kujipanga kuhakikisha chama hicho
kinashika hatamu za uongozi kuanzia ngazi ya kata hadi uraisi na kuwa
wanatakiwa kujenga umoja wenye nguvu kuweza kupambana na vyama vya
upinzani.
“Sisi ndio tunaongoza serikali
na tumefanya mengi katika kuwaletea Wananchi Maendeleo hivyo yatupasa
kutembea kifua mbele kwa kuweza kutekeleza ilani ya chama chetu kwa
asilimia mia na hii itasaidia kuweza kushinda katika uchaguzi uliopo
mbele yetu”alisema Dkta Soiley.
Aidha aliwataka wakazi wa jiji
la Arusha kujitokeza katika kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura
ilikutumia haki yao ya kikatiba, sanjari na kuipigia kura ya ndio katiba
pendekezwa,huku akiwataka wananchama wa chama hicho kujiandikisha
uananchama wao pamoja na kujitokeza kwenye ziara ya katibu mkuu wa chama
hicho.
Alisema kuwa msingi wa kuweza
kupata ushindi ni umoja kwenye chama kwani daima umoja ni ushindi hivyo
akawataka wanachama hao wa kata na wilaya kwa ujumla kuwa na umpoja na
mshikamano ili chama kiweze kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi
ujao na kura ya kuikubali katba pendekezwa.
Dkt. aliwataka wote
waliochaguliwa kuwa mabalozi wazuri wa chama kwa kuondoa kero mbali
mbali zinazoikabili jamii kwa uadilifu ilikuweza kuwajengea imani
Wananchi kukipa ridhaa sasa si wakati wa maneno bali vitendo vya
kukijenga chama kwa nguvu zetu.
Nao wenyeviti wa mitaa
ya Kaloleni kusini na magharibi wamewashukuru nwanachama na viongozi
kwa kuonyesha umoja na hatimae wao kuweza kushinda katika uchaguzi wa
serikali za mitaa hivyo wakaahidi kushirikiana na wananchi katika
kutatua kero mbali mbali.
Nae mwenyekiti wa mtaa
wa Kaloleni Magharibi Hassan Sharif alisema kuwa viongozi wa chama
lazima wawe mfano wa kuigwa na wananchi katika kuhamasisha maendeleo na
kuwataka wanachama na wakazi wa kata hiyo kuweza kushirikiana kujiletea
maendeleo sanjari na kudumisha amani na mshikamano.
habari na Mahmoud Ahmad wa libenekela kaskazini blog
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia