,
Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru)
mkoani Arusha imemhoji mkurugenzi mkuu wa kituo cha zana za kilimo na
teknolojia vijijini (Carmatec),Elfariji Makongoro pamoja na baadhi ya watumishi wa taasisi hiyo
kutokana na sakata la ufisadi wa majengo
mawili makubwa yaliyopo ndani ya taasisi hiyo.
Majengo hayo
ni yale yanayotazamana mkabala na
kiwanda cha kutengeneza matairi cha General Tyre cha jijini Arusha ambapo taasisi hiyo
iliyafungulia zabuni mwaka jana kwa ajili ya kuyapangisha
mwaka juzi lakini katika hali isiyo ya
kawaida mara baada ya kutangaza kwa washindi wa zabuni hizo na malipo kufanyika mchakato huo ulisitishwa
ghafla.
Hadi sasa
majengo hayo yako wazi kufuatia washindi
wa zabuni hizo kufungua shauri lao
mahakamani wakitaka kulipwa fedha walizolipa kwa ajili ya kupangisha ndani ya majengo hayo ambazo ni zaidi ya $ 10,000 sawa na zaidi ya sh,15 milioni.
habari na mdau wa libeneke la kaskazini Moses
Mashalla