Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha vijijini
,Fidelis Lumato amesemakuwa wilaya yake imepanga bajeti ya kiasi cha shilingi
bilioni 42 kwa mwaka wa fedha 2015 /2016
ambazo zitaelekezwa kwenye masuala ya maji,afya na elimu ili kuhakikisha
upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii.
Fidelis Lumato aliyasema hayo jana katika kikao cha
Halmashauri hiyo kilichojadili bajeti hiyo jana ambapo amefafanua kuwa mambo
hayo matatu ni vipaumbele muhimu kwa halmashauri hiyo.Amesema kuwa fedha hizo
zitasaidia kuboresha maabara,mabweni pamoja na kujenga vituo vya afya karibu.
Lumato amesema kuwa upatikanaji wa fedha hizo utasaidia
ujenzi wa barabara ya Redio Habari Maalumu,Ngaramtoni,Seliani na Sambasha
ambazo pia ni ahadi za Raisi Jakaya Mrisho kikwete.
Naye Mbunge wa Arumeru Magharibi Goodluck Ole Medeye amesema
kuwa ni vyema halmashauri ikajikita zaidi kuboresha shule za msingi na
sekondari ikiwemo shule ya Sekondari
Sokon 2 ambayo inakabiliwana uhaba wa matundu ya choo.
Medeye amewataka wananchi na madiwani kuwa wavumilivu baada
ya mashimo ya nguzo kuchimbwa kwenye
maeneo yao bila kuwekewa umeme kwanimradi wa umeme vijijini (REA) bado uko kwenye utekelezaji hadi
utakapofikia kikomo juni 30 mwaka huu.
“Nawaomba madiwani na wananchi muwe wavumilivu
badonafuatilia juu ya mradi wa REA bado wanaendelea na utekelezaji kwasasa kasi
yaoinaenda kadiri wanavyopata fedha serikalini” Alisema Medeye
Diwani
wa Kata ya Mwandeti Boniface Tarakwa amesemakuwa bajeti hiyo ilenge
kukarabati barabara ambazohazipitiki hasa kipindi cha mvua ili kuboresha
miundombinu .