Mwanamuziki Dully Sykes akihojiwa na wanahabari (hawapo pichani) huko msibani Kawe Beach jijini Dar.
Dully akilia kwa simanzi wakati akipewa pole na waombolezaji waliofika msibani Mbezi Beach, Dar leo mchana.
Mzee Sykes alifariki dunia jana mchana akiwa katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa
vidonda miguuni vilivyopelekea kueneza sumu katika mwili wake na
kumsababishia mauti.
Kwa mujibu wa Dully, Mzee Sykes alikuwa akisumbuliwa na vidonda hivyo
vilivyoshindwa kupona kutokana na kuvuta sigara. Lakini mbali na hilo
hakuwa na tatizo lingine lolote.
Mzee Sykes amefariki akiwa na umri wa miaka 62 alizaliwa Februari 24, 195