Benki ya NMB imetoa msaada wa madawati 40 na meza za walimu wenye thamani ya sh. milioni 5 katika shule za msingi Mwaramu,iliyomo wilayani humo,huku msaada huo ukiwa umetokana na faida inayopata benki hiyo.
Akiongea baada ya kukabidhi msaada huo,meneja wa benki hiyo
kanda ya kaskazini, Vicky Bishubo alisema benki hiyo imeamua kutoa
msaada wa madawati hayo baada ya kuona shule nyingi zikikosa madawati na
wanafunzi wake wakikaa chini kwenye sakafu.
Alisema
kutokana na hali hiyo wanafunzi wengi wamekuwa hawazingatii masomo
pindi wawapo darasani kwa sababu ya ukosefu wa vitendea kazi vya
madarasani hususani madawati.
‘’leo
benki ya NMB imeamua kutoa msaada wa madawati 40 , meza za walimu na
viti wenye thamani ya shilingi milioni 5 ,tumeamua kufanya hivyo
kutokana na uhitaji wa shule husika napenda niwahakikishie kuwa benki
yenu imetenga zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kuirudishia jamii
faida kidogo inayopata’’alisema Bishubo
Bishubo
aliongeza kuwa,benki hiyo iliamua kutoa msaada wa madawati hayo ya
wanafunzi ili kuweza kutoa motisha kwa wanafunzi hao kuweza kusoma kwa
bidii kwa madai kuwa kutokuwepo kwa vitendea kazi mashuleni ni moja ya
sababu zinazopelekea wanafunzi wengi kufeli.
"Msaada huu wa madawati umetokana
na faida kidogo ambazo benki inapata hivyo tumeona katika faida hizo ni
jambo jema kutoa msaada wa aina hii kwa ajili ya kuweza kuendeleza
watoto kielimu kwani wao ndiyo Taifa la kesho," alisema Bishubo.
Naye Meneja wa NMB tawi la Hai Merdadi Malisa alisema benki hiyo imejipanga kusaidia jamii katika
wilaya hiyo kwa kutoa msaada pindi inapohitajika na kuwataka wananchi
kufungua akanti katika benki hilo ili kuiwezesha benki hiyo kupata faida
zaidi.
Kwa
upande wake Mkuu wa Hai , Novatus Makunga aliipongeza benki ya NMB kwa
kutoa msaada huo na kuwataka wadau wengine wa elimu kuiga mfano wa benki
hiyo kwa kutoa mchango kama huo ili kupunguza ya madawati wilayani huo.
Alisema
wilaya ya Hai inakabiiwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu
wa madawati hata hivyo alisema taitizo hilo lipo kwa baadhi ya shule za
msingi na wilaya ipo kwenye mkakati wa kukabiliana nalo.
‘’Changamoto
ya madawani ipo sana katika wilaya yetu ya Hai ila tunajitahidi
kukabiliana nayo kwa kuwatumia wadau mbalimbali hususani nyie wa NMB
,najua benki itakuwa imepokea maombi mengi lakini tunawapongeza kwa
kuona umuhimu wa kutoa katika shule ya msingi Mwaramu iliyopo wilaya
yangu,alisema
Aliwataka
wadau wengine wa elimu kuiga mfano wa benki ya NMB,kwa kuisaidia
serikali kupunguza changamoto zilizopo kwenye shule mbalimbali hapa
nchini hasa za msingi ambako ndiko tatizo kubwa lilipo.
‘’Kupatikana
kwa madawati haya naimani kutaongeza ari ya ufaulu kwa wanafunzi
sambamba na walimu kuongeza ari ya ufundishaji katika shule hii’’alisema
Makunga
habari hii kwa hisani ya libeneke la kaskazini blog
habari hii kwa hisani ya libeneke la kaskazini blog