Makamo
mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU e.V Mheshimiwa Peter
Kazaura
Makamo mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU e.V Mheshimiwa Peter Kazaura kuwasili nchini Tanzania leo 02.02.2015 kwa ajili ya kufanya mazungumzo na kiongozi wa juu wa Taifa. akiwa Tanzania atafanya mazungumzo na uongozi wa mashirika yafuatayo TIC, Basata, Wizara ya Ardhi, NSSF, NHC, Tanzania Diaspora Initiative na Wizara ya Utamaduni Michezo na Vijana.
Mazungumzo hayo yatalenga upatikanaji wa Fursa zilizopo Tanzania kwa Diaspora. akiendelea kueleza msemaji wa Umoja huo Watanzania wanaoishi ujerumani wangependa pia kuhusishwa kikamilifu katika shughuli za maendeleo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na Afya, Elimu.
naye Mwenyekiti wa Umoja huo Mhe. Mfundo Peter Mfundo alithibitisha kuwepo kwa safari ya Makamo Mwenyekiti Mhe Peter Kazaura na alisema UTU e.V umechukua uamuzi huo baada ya Watanzania nchini Ujerumani kukosa nafasi ya kuongea na Rais wa Tanzania wakati wa ziara ya Rais nchini Ujerumani.
Pia watanzania wanaoishi ujerumani wanaulalamikia ubalozi kuwa viongozi wa umoja wao walinyimwa nafasi ya kuonana na kumsalimia Mhe.Rais Dkt.Jakaya Kikwete.