SEREKALI YA WANAFUNZI CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM-SO) YAKANUSHA KUMPIGIA DEBE LOWASA.




Serikali ya wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFMSO), kupitia
msemaji wake mkuu ambaye ni Rais wa Serikali ya wanafunzi, ndugu
Clinton Boniface inakanusha taarifa zilizotolewa na gazeti la NIPASHE
toleo namba 0578395 la tarehe 19/02/2015, lenye kichwa cha habari
“WANAFUNZI WA IFM WAMTAKA LOWASA URAIS” na kwamba habari hizo
hazijatolewa na uongozi wa IFMSO, wala hakuna mkutano wowote
uliofanyika katika eneo la chuo cha usimamizi wa fedha kati ya
waandishi wa habari na uongozi wa serikali ya wanafunzi na kutoa tamko
hilo. Pia, kulingana na Katiba ya IFMSO kifungu namba 3, ibara ndogo
ya 1, Katiba inakataza serikali ya wanafunzi (IFMSO) kushiriki katika
mambo yoyote ya kidini au kisiasa, hivyo basi IFMSO inasikitishwa na
taarifa hizo na inaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza
kutokana na taarifa hizo.

Imetolewa na;

…..........
Clinton Boniface.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi.
IFM-SO
19/ 02/ 2015.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post