Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Felix
Ntibenda akimkabidhi godoro mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Engutoto kama
msaada baada ya kuunguliwa na bweni.
Alice Mapunda, Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha
alifika katika shule hiyo nakujionea maafa hayo yaliyotokea katika shule hiyo.
Mkuu wa Mkoa awaomba watu mbalimbali walioguswa
na tukio hilo kutoa msaada wa vitu mbalimbali ilikuwasaidia wanafunzi hao
waweze kuendelea na masomo yao.
Baadhi ya wadau walioguswa na tukio
hilo wametoa magodoro 180, mashuka 360 na pesa taslimu kiasi cha shilingi
milioni 25 kwa wanafunzi hao walionguliwa na bweni.
Chanzo cha moto huwo ilikuwa ni shoti
ya umeme iliyopelekea bweni lote la
kidato cha nne kuungua na kuteketeza kila kitu katika bweni hilo.
Moto huwo ulitokea kipindi wanafunzi
wote walipokuwa wakijisomea madarasani na hivyo hakuna mwanafunzi yoyote
aliyejeruhiwa.