picha ya bondia Francis Cheka
Bondia
maarufu nchini wa ngumi za kulipwa Francis Cheka amehukumiwa kifungo
cha miaka 3 jela na kutakiwa kulipa fidia ya shilingi millioni 1 kwa
kosa la kumpiga na kumjeruhi meneja wa baa yake iliyopo huko Morogoro
Meneja
huyo ajulikanaye kwa jina la Bahati inaelezwa alienda kudai fedha zake
alizokuwa hajalipwa na bondia huyo wakati akifanya kazi ya umeneja
katika baa yake hiyo ndipo Bondia huyo alikataa kumlipa na kumshushia
kipigo