Weasel na Radio
Mastaa wa
muziki kutoka nchini Uganda, Radio pamoja na Weasel wameelezwa kuwa
katika mpango wa kusaka meneja mpya ambaye ataenda nao sawa na
kuhakikisha anawaweka sawa katika kuimarisha soko la muziki wao nje ya
mipaka ya nchi hiyo.
Hatua hii
imeelezwa kuwa ni kutokana na kitendo cha Meneja wao wa sasa
anayefahamika kwa jina Chagga kuteleza na kuingia katika ugomvi na
mashabiki wa wasanii hawa, kitendo ambacho wanahofia kuwachafulia jina
na kuyumbisha biashara yao ya muziki.
Wasanii
hawa pia wameweka mkakati huu kwa lengo la kwenda sawa na kasi ya
ushindani ya muziki ambao sasa umekuwa na unahitaji kusambaa kwa kasi
nje ya mipaka ya nchi yao.