KAIMU MKURUGENZI WA TPA MADENI KIPANDE ASIMAMISHWA KAZI

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta (pichani kulia akizungumza na wanahabari leo bandarini) amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), Eng Madeni Shamte Kipande kwa tuhuma za utendaji mbovu, ikiwa ni pamoja na kutokuwepo kwa uwazi kwenye mamlaka hiyo hususani katika michakato ya zabuni mbalimbali zinazotangazwa na mamlaka hiyo.

Pamoja na kuchukua uamuzi huo Mhe. Sitta, ameunda tume ya watu sita itakayokuwa na jukumu la kuchunguza tuhuma zinazomkabilia Mhandisi Kipande ambaye atakuwa nje ya madaraka kwa muda wa wiki mbili kupisha uchunguzi huo na nafasi yake itakaimiwa na Meneja wa Bandari Dar es Salaam Bw. Awadhi Masawe.
Kipande aliteuliwa kushika wadhifa huo mnamo mwaka 2012 mwezi Agosti na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe. 

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post