Msanii wa
muziki Peter Msechu amesema kuwa, baada ya ngoma yake ya Nyota kufanya
vizuri nnje ya mipaka ya nchi hususan huko Nigeria amegundua kuwa
melody,ubora na mpangilio wa vyombo mara nyingi ndio kitu pekee ambacho
huvuta watu kupenda wimbo.
Amesema watu wanapenda melody na si ujumbe uliopo ndani yake na kuwezesha rekodi husika kufanya vizuri hata nje ya mipaka.
Msechu
amesema kuwa, kuna haja ya wasanii wa hapa nyumbani kushikilia misingi
ya muziki wa hapa nyumbani na kuzingatia vitu hivi huku kukiwa na
uwezekano mkubwa wa kuvuka mipaka endapo rekodi ambayo mtu atafanya
itakuwa na ubora na midundo na melody ya kuvutia.