DJ Tee (19) ni
kijana mwenye ndoto kubwa katika maisha yake. Baada ya kuona mahangaiko ya
vijana kuelekea kwenye mafanikio, wengi wakiwa wamemaliza shule na vyuo
bila kupata kazi, ameamua kuunda redio stesheni ghetoni kwake aliyoipa jina
la Shujaaz, ili aweze kushea ideas na vijana wote nchini Tanzania kuhusu
mbinu mbalimbali za kuingiza pesa, kuwapa stori za vijana wanaochakarika
katika maisha yao pamoja na kuwaburudisha.
"Nimeamua
kuiita Shujaaz kwa sababu, naamini kuwa kijana ambaye anajituma na kuweka
mfano bora kwenye jamii ni shujaa". Alisema DJ Tee. "Ndoto zangu
zinakaribia kuwa kweli".
Story ya
kijana huyu inapatikana kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kupitia kijarida
cha Shujaaz, kitakachokuwa kinasambazwa kupitia gazeti la Mwanaspoti,
kuanzia JUMAMOSI HII ya tarehe 28. Kwenye kijarida hicho, utapata ideas
mbali mbali ambazo vijana wanaweza kuzifuata na kujiingizia kipato. Pia,
kutakuwa na stori za vijana wengine kama Pendo, Semeni na Pepe ambao ni
mashabiki wakubwa wa DJ Tee na redio show yake ya
Shujaaz.
DJ
Tee akiwa studio.
Kijana huyu
ameamua kujiita DJ Tee ili asijulikane na watu wake wa
karibu, kwa kuwa ana-hack airwaves za redio stesheni ili aweze kusikika.
Sikiliza redio stesheni uipendayo kuanzia wiki ijayo, huwezi jua,
inawezekana DJ Tee akawa hewani!
Wewe pia
USIKOSE kuwa sehemu ya mafanikio na harakati za kijana huyu kwa kujiunga
naye. Pata nakala yako ya Shujaaz kuanzia Jumamosi hii (28/02/2015) kupitia
gazeti la Mwanaspoti. Pia, jiunge naye kwenye ukurasa wake wa Facebook kwa
jina DJTee255 ili upige naye story na wewe uweze kushea
idea zako za hustle. Unaweza pia ukampata Instagram na Twitter kwa jina
@djtee255
Studio.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia