MBIO ZA KILIMANJARO MARATHON ZAZINDULIWA RASMI MKOANI KILIMANJARO MJINI MOSHI



KILIMANJARO Mashindano ya  13 kimataifa ya riadha ya Kilimanjaro marathoni  mwaka  2015 ya mezinduliwa rasmi mkoani Kilimanjaro ambapo Tanzania imetamba kuwa  itag’ara katika mashindano  hayo yanayo tarajiwa kufanyika mwezi machi mwaka huu mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza  kwa niaba ya raisi wa chama cha riadha nchini kwenye uzinduzi wa mashindano hayo uliyofanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, mwenyekiti wa chama cha riadha mkoani Kilimanjaro Listone Metacha alisema Tanzania imewaanda  vilivyo wachezaji wake  mapema badala ya kukurupuka katika dakika za mwisho.
Akizindua mbio  hizo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro leonidas Gama, katibu tawala wa mkoa  wa Kilimanjaro Severin Kaitwa, amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika kushiriki mashindano hayo, ambayo  mbali na kuchangia uchumi wa nchi ya Tanzania, pia yanaipa sifa kubwa kimataifa.

Meneja wa bia ya Kilimanjaro ambayo ni mdhamini mkuu wa mashindano hayo  Pamela Kikuli, alisema kwa miaka 13 sasa wamekuwa wakidhamini mashindano hayo, ambapo mwaka huu  wametenga  kiasi cha shilingi milioni 20, kwa washindi 10 wa mbio ndefu za kilometa 42, ambapo washindi wa kike na wa kiume kwa mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha shilingi milioni nne na mshindi wa pili  atanyakua shilingi milioni mbili huku mshindi watatu kwa upande wa wanaume na wanawake wataondoka na shilingi milioni moja kila mmoja.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post