Mwenyekiti wa Chadema Freman Mbowe akiwa anasoma utuba wakati wa ufunguzi wa mkutano wa viongozi wa chama hicho wa kanda ya kaskazini unaofanyika leo katika hotel ya new Arusha jijini hapa |
viongizo wa chadema akiwemo mwenyekiti wakiwa wanasali kwanza kabla ya mkutano wa viongozi wakanda ya kaskazini kuanza
Naibu katibu mkuu wa Chadema Salum Mwalimu akiwa anaongea nawaandishi wahabari
MWENYEKITI wa chama cha demokrasi na maendeleo Chadema Freeman Mbowe amesema kuwa chama chao kimejipanga kuahakikisha kinahamasisha kwa nguvu zote wananchi weweze kwenda kujiandikisha katika daftari la mpiga kura
Alisemakuwa hii itaweza kumsaidia kila mwananchi kuweza kupata haki yakumchagua kiongozi bora anaemtaka katika uchaguzi mkuu ujao wa kuwachagua viongozi wakuu ambao ni rais ,wabunge na madiwani.
Alisema kuwa pamoja ya kuwa tume wamekuwa wananchelewesha kufanyika kwa zoezi hili , wao wamejipanga kikamilifu na pindi ambapo zoezi hili litatangazwa kuanza rasmi watajitaidi kwa njia yoyote kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha
Alisema kuwa kwa upande wa kupiga kura katiba wanaendelea na msimamo wao ambao walitangaza awali wa kutoshiriki katika mchakato wa kura
ya maoni ya katiba huku akisisitiza kuwa swala la kutoshiriki katika mchakato wakura za maoni auingiliani kabisa na kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura
Alimaliizia kwa kuwasihi wananchi wajitokeze kwa wingi sana pindi pale ambapo watasikia zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu limewadia ili waweze kupata haki yao ambayo itawaruhusu kuchgua kiongozi wanao wataka.