Acha kabisa! Mazishi ya baba wa mastaa wa muziki wa Nigeria, mapacha Peter na Paul Okoye wanaounda ‘Kruu’ ya P-Square, Moses Okoye aliyefariki dunia Novemba 24, 2014 yamefanyika kama sherehe siku ya Ijumaa januari 30 mwaka huu. |
Ishu
hiyo ilijiri nyumbani kwa mastaa hao eneo la Ifitedunu, Jimbo la
Anambra nchini humo Ijumaa iliyopita ikiwa ni siku 65 tangu mzee huyo
alipofariki dunia baada ya kufanyiwa oparesheni ya goti alipodondoka
kwenye ngazi nyumbani kwake maeneo hayo.
Tofauti
na ilivyozoeleka kwamba kwenye msiba watu huwa wanalia na kuomboleza,
mazishi hayo yaliyohudhuriwa na mastaa kibao nchini humo yalikuwa
tofauti kwani watu walikuwa na nyuso za tabasamu huku wakiserebuka na
matarumbeta juu.
Ulinzi mkali ukiimarishwa katika msiba huo.
Mbali
na kuonekana kuwa kama sherehe, pia mazishi hayo yaliripotiwa kuwa ya
gharama zaidi kuanzia jeneza lililobeba mwili wa baba yao, gari ‘spesho’
lililokuwa na jina la Dady badala ya namba za usajili na wahudhuriaji
waliopiga sare nyeupe huku wakijifotoa picha wakicheka na kutupia kwenye
mitandao ya kijamii.
Mwili wa baba wa P-Square ukiwa kwenye jeneza.
Pia
kivutio kikubwa kilikuwa ni wake wa mastaa hao ambao walipewa ulinzi
mkali uliowekwa katika mazishi hayo yaliyohudhuriwa kwa mualiko maalum.
Baba wa P-Square (aliyenyosha mikono) enzi za uhai wake.
Cha
kushangaza, wakati mwili wa baba yao ukiwa mochwari, jamaa hao
walidaiwa kuendelea na ratiba za kimuziki huku wakifanya shoo kama kawa
jambo ambalo kwa Bongo haliwezekani.
Kwa sasa mastaa hao hawana mzazi hata mmoja baada ya mama yao naye kufariki dunia mwaka 2012.
Kwa sasa mastaa hao hawana mzazi hata mmoja baada ya mama yao naye kufariki dunia mwaka 2012.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia