MKUU wa
Mkoa wa Arusha, Davidi Ntibenda
Alice
Mapunda, Arusha.
MKUU wa
Mkoa wa Arusha, Davidi Ntibenda, amewaagiza wakuu wa wilaya zote mkoani humo, kuhakikisha
watoto wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu, wawe
wamesharipoti haraka iwezekanavyo
ifikipo Februari 28.
Kaulo hiyo
ameitoa wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa kata za Loliondo
na Sale, alipofanya ziara katika wilaya ya Ngorongoro nakuongea na wananchi wa
kata hizo.
“Napenda
kuwaagiza wakuu wa wilaya zote za mkoa huu, kuhakikisha kila mzazi ambae mtoto
wake amefaulu kuingia kidato cha kwanza kumpeleka shuleni mapema iwezekanavyo.
Naomba nipewe taarifa kamili ifikapo Februari 28, mwaka huu,” alisema Ntibenda.
Alisisitiza
kuna tatizo kwa baadhi ya wazazi kuwakatiza watoto wao masomo kwa kuwaozesha au
kuoa pindi wanapopata nafasi zakuendelea na masomo yao ya Sekondari,hivyo
kupelekea kuwa na ndoa na mimba za
utotoni.
Pia Ntibenda
alitoa ovyo kali kwa walimu wote kutowatoza pesa wazazi watakaofika mashuleni
kuwaandikisha watoto wao kwa ajili ya elimu ya msingi.
Alionya
kuwa kufanya ivyo ni kukiuka taratibu za uwandikishaji kwa mfumo wa elimu
uliopo.
“Hii
inasababisha wazazi wengine kushindwa kumudu gharama hizo kusababisha watoto
wao kushindwa kujiunga na elimu ya msingi,” alisisitiza.
Mbali na
hayo alitoa msisitizo kwa walimu na wazazi kuwahamasisha watoto
wao wapende masomo ya Sayansi
ilikuandaa wataalamu wakutosha katika sekta hiyo.
Mkuu wa mkoa,
yupo katika ziara maalumu kwa wilaya zote kwa lengo la kutoa shukrani kwa
wananchi wa mkoa wa Arusha kwa uteuzi wake kama mkuu wao.
Aliomba ushirikiano
kutoka kwa wananchi wote ili kuleta
maendeleo ya mkoa huo
kwa ujumla na kukagua ujunze wa maabara ambao bado unaendelea katika mkoa
mzima.