CHAMA
cha Wakulima Tanzania (TFA), kimepata hasara ya sh bilioni 5 kwa
kipindi cha miaka 10 mfululizo kutokana na viongozi wa bodi kuwa na
matumizi mabaya ya fedha na kujiidhinishia mali za ushirika kama zawadi
hali iliyosababisha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Utawala, Elias
Mshiu kufukuzwa na wanachama katika mkutano mkuu maalumu.
Mshiu anadaiwa kujiidhinishia nyumba kubwa ya kisasa iliyopo barabara ya Haile Selasie kiwanja namba 57 kilichopo katikati ya Jiji la Arusha na baadaye kuomba kupewa nyumba hiyo kama zawadi pamoja na mafao ya sh milioni 65 mara baada ya kustaafu.
Mwenyekiti wa kamati iliyoundwa na wanachama kuchunguza TFA, Maynard Swai, alibainisha hayo katika taarifa yake aliyoisoma katika mkutano mkuu maalumu wa chama hicho uliofanyika juzi jijini hapa.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na wajumbe zaidi ya 520 kutoka mikoa yote nchini, wajumbe waliazimia kwa kauli moja kufukuzwa kwa mwenyekiti na mkurugenzi wa bodi na utawala wa TFA aliyedumu madarakani kwa zaidi ya miaka hamsini.
Swai alisema TFA imepata hasara za mfululizo mwaka hadi mwaka kutokana na Mshiu kuwa na nyadhifa mbili kwa wakati mmoja – ‘kuvaa koti la mkurugenzi mtendaji na mwenyekiti TFA’ kwa kipindi kirefu, na hivyo kuwa na mamlaka ya kusaini mikataba na ajenda za vikao peke yake bila ya kuwapo kwa katibu mtendaji wala wakaguzi wa mahesabu wa ndani na nje.
Alisema kuwa matumizi mabaya ya madaraka yamesababisha hasara kubwa kwani viongozi wa bodi na utawala wamekuwa na matumizi makubwa kuliko mapato, huku akijiingiza katika kuchukua mikopo mikubwa kwa riba kubwa na kushindwa kulipa, na hata kuwalipa wazabuni wanaosambaza pembejeo.
Kamati hiyo pia ilimtuhumu mwenyekiti kujiidhinishia malipo makubwa ya mshahara, posho na masurufu kibao licha ya kwamba kila mwezi alikuwa akilipwa mshahara wa dola 1,000 za Kimarekani sawa na zaidi ya sh milioni 1.6 za Kitanzania, huku wanachama wakikosa gawio na mapato ya chama yakididimia kila mwaka.
Mshiu pia anatuhumiwa kumiliki kampuni binafsi ya ulinzi ya Apex Security Service Ltd na kampuni inayojihusisha na usafi wa mazingira, Aresco na kujipa tenda ya ulinzi na usafi katika makao makuu ya TFA bila kufuata taratibu za sheria ya manunuzi na ugavi za shirika ama serikali, na hivyo kuendesha TFA kama mali ya familia.
“Mwenyekiti ameshindwa kuzingatia misingi ya utawala bora kwa kushika nyadhifa mbili kwa wakati mmoja kwa kipindi cha miaka mitano, kwani aliajiri kampuni ya ulinzi wakati ana hisa katika hiyo kampuni na hakuweka wazi maslahi yake, na hivyo kamati imeona Mshiu aliweka maslahi yake binafsi mbele kuliko TFA,” alisema Swai.
Kamati hiyo ya uchunguzi ilibaini kushindwa kwa mwenyekiti wa bodi na mtandao wake kuinusuru Kampuni ya TFA na kuisababishia hasara ya mabilioni ya fedha, na hakuna hatua endelevu alizozichukua ili kuinusuru wala uwajibikaji kwa wajumbe wa bodi na utawala.
Katika mkutano huo, wajumbe waliazimia kwa kauli moja kuwa mwenyekiti airejeshe nyumba na magari ya kifahari aliyojimilikisha bila mkutano mkuu hatua iliyopingwa na Mshiu kwa madai kwamba nyumba ya Haile Selasie alipewa kihalali na kukabidhiwa nyaraka zote kisheria na bodi ya wakurugenzi kama zawadi ya kuongoza chombo hicho kwa zaidi ya miaka hamsini.
Mshiu alisema alianza kazi TFA akiwa na umri wa miaka 18 na baadaye kusomeshwa hadi chuo kikuu, huku akiwa ameikuta TFA na mtaji wa sh milioni 200, na sasa ameondolewa madarakani kibabe huku akiwa ameacha mtaji wa zaidi ya sh bilioni 22 na matawi 12 nchini nzima.
“Nimetolewa kutokana na uchu tu wa madaraka, wameona TFA imesimama kwa zaidi ya miaka 50, lakini kuna mashirika mengine kama ACU na mengine ya umma yamekufa. Kutokana na jitihada zangu wameona TFA imesimama na kuniondoa kwa kunidhalilisha madarakani kwa hila tu,” alijitetea Mshiu.

Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia