Mtoto Clara Damian mwanafunzi wa darasa la saba asiyeona akiwa darasani
akitumia mashine maalumu ya kuandikia na kusoma katika shule ya msingi
patandi iliyopo wilaya ya arumeru mkoani arusha shule hiyo inakabiliwa na
upungufu wa walimu na vitabu.
akitumia mashine maalumu ya kuandikia na kusoma katika shule ya msingi
patandi iliyopo wilaya ya arumeru mkoani arusha shule hiyo inakabiliwa na
upungufu wa walimu na vitabu.
Na Woinde Shizza,Arusha.
Wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya msingi Patandi iliyopo wilaya
ya Arumeru Mkoani Arusha wamelalamikia tatizo la upungufu wa
walimu,vitabu na vifaa vya kufundishia kwa wanafunzi hao wenye
mahitaji maalumu hali inayokwamisha maendeleo ya kitaaluma hivyo
wameiomba serikali na taasisi binafsi kutatua changamoto hiyo.
Mwanafunzi asiyeona anayesoma darasa la saba Clara Damian ni alisema
kuwa kumekua na uhaba wa vitabu kwa watoto wasioona na mashine za
kuandikia maandishi yenye nundu ambazo ni chache na kwa sasa ni
mashine tatu pekee zinafanya kazi ukilinganisha na idadi kubwa ya
wanafunzi.
Alisema kuwa miundombinu ya majengo ya madarasa pia yamekua si rafiki
kwa watoto wenye ulemavu hivyo anashauri miundombinu ya majengo na
shule iendane na mahitaji wa watoto hao.
Mibaku Limba Mwanafunzi asiyesikia (kiziwi) alisema kuwa walimu
walioko kwa sasa wanaofundishwa kwa lugha za alama ni wachache
ukilinganisha na idadi ya masomo hali ambayo inachangia kuwarudisha
nyuma.
Mratibu wa Kitengo Cha Walemavu Mwalimu Anna Shayo Katika Shule hiyo
Mwalimu Shayo alikiri kuwepo kwa upungufu wa walimu na vitabu kwa
watoto wenye mahitaji maalumu na kuiomba jamii,taasisi na serikali
kushiriki katika kuboresha maendeleo ya watoto hao ambao wakijengewa
misingi bora ya elimu wanaweza kuwa na mchango kwa jamii badala ya
kuwa tegemezi.
Mwalimu Marko Alois Mamuya anayefundisha watoto viziwi ameiomba
serikali itoe motisha kwa walimu wanaofundisha watoto wenye mahitaji
maalumu ili kuongeza ari na hamasa itakayosaidia kupata idadi kubwa ya
walimu .
“Tunawaomba wazazi wasiwafiche watoto wenye ulemavu majumbani bali
wawalete mashuleni huku waweze kupata elimu ,lishe na mazoezi badala
ya kuwafungia nyumbani kwani wanazidi kuwa tatizo licha nya
uwezo,vipaji na ubunifu walioanao ambao unaweza kuwasaidia wao na
jamii yao” alisema Mwalimu Marko