MAONESHO ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu
Sabasaba, yanatarajiwa kufunguliwa leo na Rais wa Rwanda, Paul Kagame,
ikiwa ni maonesho ya kwanza ya mpango wa pili wa miaka mitano ya ujenzi
wa uchumi wa viwanda nchini.
Kutokana na uzinduzi, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles
Mwijage amewahimiza wananchi kufika kujifunza uanzishaji wa viwanda vidogo,
kati na vikubwa.
Akizungumzia ufunguzi huo, Mwijage alisema katika maonesho hayo wenye
ndoto za kuanzisha viwanda hawana budi kufika kujifunza namna ya kujenga
viwanda kwa fedha kidogo wakiungwa mkono na taasisi za kifedha.
Alisema maonesho hayo yanayoshirikisha nchi zaidi ya 30 yatatumika
kurasimisha biashara kwa kutumia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni
(BRELA) kwa muda mfupi.
“Brela itakuwepo kuonesha kuwa Tanzania ina uwezo wa kusajili kampuni kwa
muda mfupi isipokuwa mtu awe na nakala muhimu,” alisisitiza.
Alisema katika kuonesha maonesho hayo yamejikita kujengea uwezo
Watanzania kuanzisha viwanda vinavyozalisha bidhaa bora kuna banda
maalumu lenye wataalamu wa viwanda na uwekezaji watakaotoa maelekezo ya
viwanda na uwekeza