picha ikionyesha wa kwanzakushoto ni Afisa ustawi wa jamii ambaye pia ni msimamizi wa mahabusu ya watoto mkoa wa Arusha Mussa Mkamate akiwa anabadilishana jambo na baadhi ya wajumbe wa Jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Arusha mara baada yakukabidhi magodoro kama msaada wa mahabusu hayo
Na Woinde Shizza , Arusha
Kamati ya utekeleza
ya wazazi wa CCM wilaya ya Arusha
leo wamekabidhi jumla ya magodoro 25 katika mahabusu ya watoto iliyopo
jijini hapa ikiwa ni ahadi walioiweka ya kusaidia baadhi ya changamoto zilizopo
katika mahabusu hiyo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi magodoro hayo mmoja wa
wajumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni meneja masoko wa Radio ya Triple A iliopo
jijjini Arusha Phidecia Mwakitalima
alisema kuwa hii ni mara ya tatu wao kama kamati ya wazazi wa wilaya kukabidhi msaada huo kwani
mara ya kwanza walishatoa chakula na mashuka kwa ajili ya watoto hao na sasa
hivi wameamua kuwaletea msaada wa magodoro.
Alisema kuwa magodoro hayo 25 yametokana na msaada ambao wao
kama kamati ya wazazi waliuomba kwa wadau mbalimbali ambapo katika wadau hao
kampuni ya magodoro ya Tanform iliopo arusha iliwaunga mkono na kuamua kuwapa
magodoro hayo kwa ajili ya watoto hao wa mahabusu ya watoto Arusha.
Aidha Phidecia alimalizia kwa kutoa wito kwa wadau
mbalimbali ,wafanyabishara ,viongozi
pamoja na wananchi kujijengea
tabia ya kutembelea mhabusu mbalimbali za watoto zilizopo hapa nchini ili kuweza kugundua changamoto walizo nazo watoto
hao na kuweza kuwasadia kuzitatua ikiwa ni pamoja na kuwapa baadhi ya mahitaji
ambayo watoto hao walioko mahabusu hawayapati
pamoja na kutatua kero walizo nazo.
Naye mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Arusha Ally Mtumwa alisema kuwa juhudu za jumuiya ya
wazazi CCM wilaya ya Arusha hazitaishia hapo
kwani huu ni mwanzo wataendelewa kuwasadia watoto wa mahabusu hii pamoja
na watoto wengine wanao ishi katika mazingira magumu na wale yatima waliopo
ndani ya mkoa wa Arusha.
Alisema wao kama wazazi wanaguswa sana na baadhi ya matatizo yanayowapata watoto hao wanaoishi
katika mahabusu hii ya watoto pamoja na wale wanaoishi katika mazingira magumu
hivyo watajitaidi kwa kila njia kuwasadia .
“hii sio mara ya kwanza
kuwasadia watoto hawa na wala sio watoto hawa tu tunawasaidia na pia atutaishia hapa tutaendelea kuwasaidia
watoto hawa sisi kama wazazi adi pale tutakapoona sasa watoto hao wanaishi
katika hali nzuri kama wale watoto wana wazazi wanaoishi majumbani kwao.
Kwa upande wake katibu wa wazazi CCM wilaya Arusha Rehema Mohamed alisema kuwa mara ya kwanza walipotembelea katika mhabusu
haya walikuta magodoro yamechakaa ,eneo limechakaa,watoto wanaishi katika
mazingira magumu ,vyoo vya mahabusu hiyo vilikuwa vibovu pamoja na mahabusu
hiyo kutokuwa na chakula cha kutosha kwa ajili ya watoto hao lakini wao kama
jumuiya walishirikiana kutafuta wadau ambao wamejitokeza kusaida kutatua baadhi ya
changamoto ikiwa ni pamoja na kupeleka chakula,mashuka ambayo hayakuwepo sasa
ivi wamempata huyu ambaye aliwapelekea magodoro na wao wameyachukuwa na
kuyakabidhi katika mahabusu hiyo.
“pia naomba sana
serekali ,pamoja na mahakama kwa ujumla kuangalia usikilizaji wa kesi za watoto
hawa kwani kuna baadhi ya watoto wameshakaa ndani ya mahabusu hiyo kwa muda
mrefu lakini kesi zao azisikilizwi ,na ambazo zinasikilizwa azitolewi ukumu kwa
wakati na zikitolewa ukumu watoto hao wanatakiwa kufungwa badala ya kupewa
adhabu tunaomba sana serekali hii iangalie sana kwa makini swala hili “alisema
Rehema.
Aidha alitolea mfano mmoja wa mtoto(12) ambaye alishitakiwa
kwa kosa la kuiba simu lakini ilifikia
sehemu mwenye simu alimsamehe ,na alivyopelekwa mahakamani motto huyo alikiri kosa na kutolewa ukumu afungwe miaka miwili ,kitu ambacho ni sio kizuri kwani sheria
inasema mtoto kama huyo anatakiwa kupewa adhabu na sio kufungwa.