MKUU
WAPOLISI WILAYA YA ARUSHA( SSP)EMMANUEL TILLE AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI
WA KATA YA MOIVARO TARAFA YA SUYE NA PAMOJA NA ASKARI WA ULINZI
SHIRIKISHI WAKATI WA UZINDUZI WA VIKUNDI VINNE VYA KATA HIYO.
Jeshi
la Polisi linaendeleza harakati za kupambana na uhalifu ili kupunguza
matukio ya namna hiyo, wananchi wa kata ya Moivaro tarafa ya Suye
halmashauri ya jiji la Arusha hawapo mbali na jitihada hizo hivyo kuamua
kujitokeza kwa moyo mmoja kupinga uhalifu kwa kuanzisha vikundi vinne
vya ulinzi shirikishi kutoka mitaa ya Ngurumausi, Oldonyommasi, Moivaro
Kati na Shangarao.
Akizindua
vikundi hivyo ambavyo vimewezeshwa na wadau walioongozwa na Jeff Mligha
ambao walijitolea vifaa mbalimbali vya ulinzi zikiwemo tochi, Mkuu wa
Polisi wilaya ya Arusha Mratibu Mwandamizi wa Polisi Emmanuel Tille kwa
niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha alisema kwamba matarajio ya
wananchi katika kata hiyo ya Moivaro ni makubwa na ana imani watakuwa
wanalala na kuamka salama hivyo kuwataka walinzi hao wawe na nidhamu
kwenye kazi yao.
“Kazi
ya ulinzi ina miiko yake; kitu cha kwanza ni nidhamu ya hali ya juu.
Mimi mwenyewe mpaka nafikia hatua hii ni kwa sababu ya nidhamu na
nawataka ninyi muige mfano wangu, ninachosema hapa ni pamoja na kuwahi
kazini, kutunza siri pasipo kuwazunguka wenzako pamoja na kufuata
maelekezo ya wakubwa wa vikundi vyenu” Alisisitiza Tille.
Amesema
japokuwa askari hao wapatao 42 wamepewa mafunzo lakini kupitia Wakaguzi
wa Polisi wa Tarafa na askari kata wataendelea kuwapa mafunzo mara kwa
mara ili waweze kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria, huku akiwaonya
wasijichukulie sheria mkononi.
Amewataka
wananchi wanapopata taarifa watoe kwa viongozi wa Polisi mara moja ili
ziweze kufanyiwa kazi kwa haraka na hatimaye kufikia malengo ya
kupunguza uhalifu ndani ya jiji la Arusha, huku akiwataka watendaji wa
kata na Wakaguzi wa tarafa wahakikishe askari wa kata wanakuwa katika
maeneo yao kila siku hali ambayo itawasaidia kubaini maeneo tete.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Diwani wa kata hiyo Rick Moiro alivitaka vikundi
hivyo kufuata taratibu za kazi na kupambana na uhalifu hasa vijana
wanaojihusisha na madawa ya kulevya aina ya bangi huku akiomba Jeshi la
Polisi litoe ushirikiano wa karibu na vikundi hivyo pindi tu wanapoomba
msaada.
Afisa
Mtendaji wa kata hiyo Bi. Editha Kisangia alisema kwamba mbali na hali
ya uhalifu kuwa ya kawaida katika eneo hilo lakini hatarajii kutokea kwa
changamoto kutoka kwa baadhi ya wananchi kushindwa kuchangia vikundi
hivyo kwani faida wataiona baada ya kuanza kufanya kazi.
Wakaguzi
wa Polisi wanaoongoza tarafa tatu za halmashauri ya jiji la Arusha toka
mwaka 2013 ni pamoja na Frimina Massao tarafa ya Suye, Winibrita Moshi
tarafa Elerai na Shabani Shabani tarafa ya Themi.
MKUU
WA POLISI WILAYA YA ARUSHA( SSP) EMMANUEL TILLE AKIWAKAGUA ASKARI WA
VIKUNDI VYA ULINZI SHIRIKISHI KUTOKA MITAA YA
NGURUMAUSI,OLDONYOMMASI,MOIVARO KATI NA SHANGARAO.
DIWANI
WA KATA YA MOIVARO RICK MOIRO AKIZUNGUMZA NA VIKUNDI VYA ASKARI WA
ULINZI SHIRIKISHI WALIOTOKA KWENYE BAADHI YA MITAA YA KATA YAKE BAADA YA
UZINDUZI WA VIKUNDI HIVYO.
MMOJA
WA WAHITIMU WA MAFUNZO WA VIKUNDI VYAASKARI WABULINZI SHIRIKISHI
AKIKABIDHIWA KITAMBULISHO CHA KAZI NA MKUU WA POLISI WILAYA
(SSP)EMMANUEL TILLE.
BAADHI
YA VIONGOZI WA KATA YA MOIVARO PAMOJA NA VIKUNDI VIPYA VYA ASKARI WA
ULINZI SHIRIKISHI WAKIMSIKILIZA MKUU WA POLISI WILAYA YA ARUSHA
(SSP)EMMANUEL TILLE.