Halmashauri ya jiji la Arusha imetamba kuvuka malengo ya shilingi bilioni 13 iliyojiwekea hadi kufikia Juni 30 mwaka huu , baada ya kufanikiwa kukusanya jumla ya shilingi Bilioni 10 hadi kufikia Mei 30 mwaka huu.
Hayo
yamesemwa na Meya wa Jiji la Arusha Kalist Lazaro wakati akiongea na
vyombo vya habari Ofisini kwake kufuatia agizo la raisi Dr John Pombe
Magufuli alilolitoa kwamba halimashauri itayoshindwa kufikia asilimia 80
ya lengo la kukusanya mapato yake halimashauri itafutwa.
Amelisema
kuwa mapato hayo yameweza kuongezeka maradufu tofauti na makusanyo ya
nyuma mara baada ya kufanikiwa kuziba mianya ya upotevu wa fedha
kutokana na wafanyakazi wa halimashauri hiyo walio kuwa sio waaminifu na
kupelekea makusanyo ya kodi yasiyo madhubuti .
Ameainisha
vyanzo vya mapato ambavyo wameweza kuvisimamia vizuri na kupata
mapato maradufu ni pamoja na Soko la Kwa Mromboo kuweza kukusanya
takribani Milioni 240 kwa mwezi , sambamba na kuweza kuondoa Madalali
ndani ya maduka ya halimashauri na kuwezesha halimashauri kuvuna Milioni
180 kwa mwezi.
“Tangu
nimeingia kwenye nafasi ya Umeya nimekuta katika maduka mengi yanayo
milikiwa na Halimashauri yana milikiwa na Madalali ambao hulipa
Halimashauri kiasi kidogo huku wao wakipokea pesa nyingi yakiwemo ya
Soko la Vifodi , Kwa Mromboo na Soko Kuu”, Alisema Kalisti.
Meya
huyo wa Jiji la Arusha amesema kuwa miongoni mwa mafanikio ambayo
wameyapata katika uboreshaji wa mapato hayo ni pamoja na kuweza kutoa
asilimia 10 ya mapato yote jumla ya Milioni 405 kukopesha vikundi 64
vya kina mama na vijana pamoja na miradi ya maendeleo yenye thamani ya
Bilioni 4 ikiwa ni maendeleo ya miundo mbinu ya jiji la Arusha.
Wakati
huo huo halimashauri ya jiji la Arusha imeamua kusitisha wakala wa
makusanyo ya Ushuru wa maegesho ya magari iliyokuwa imeshikwa na
kampuni JJ Mining inayomilikiwa na mfanyabiashara Justini Nyari ,
aliyekuwa akiipatia halimashauri hiyo kiasi cha shilingi Milioni 60 kwa
mwezi.
Amesema
hatua hiyo ni kufuatia agizo la serekali la kuzitaka halmashauri zote
nchini kukusanya na kusimamia mapato yake ya Ndani yenyewe bila ya
kutumia wakala , na hivyo Halimashauri hiyo imeamua kuajiri wafanyakazi
wake watakaokusanya mapato hayo.