mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa anamtisha mwanafunzi ndoo ya maji mara baada ya uzinduzi wa mradi wa maji kwa hiasani ya UNICEF walifadhiri mradi wenye thamani ya Tshs Mil 119 kwa kijiji cha Mikongati
Mfadhiri wa mradi wa Maabara katika zahanati ya Kisinga Bwana Feisal ASAS akipokea cheti cha shukrani toka kwa naibu waziri
Mh Selemani Jafo na Mheshimiwa Richard Kasesela wakishirki katika uzinduzi wa sehemu ya kunawia watoto katika shule ya Mikongati
Naibu
Waziri ofisi ya rais TAMISEMI Mh Selemani Jafo amefanya ziara katika
halmashauri ya Iringa ambapo alipokelewa na Mkuu wa wilaya ya Iringa
Mheshimiwa Richard Kasesela akiongozana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Iringa Mh Stephen Mhapa. Katika ziara hiyo alikagua miradi ya maendeleo
na kufungua miradi ya vyoo katika shule ya msingi Mikongati tarafa ya
Kalenga, maabara ya zahanati ya Kising'a na madarasa ya shule ya
sekondari Mikongati. Pia alizungumza na watumishi wa Halmashauri ya
Iringa. Katika hotuba yake Mh Jafo alisistiza suala la upendo kazini na kujenga nidhamu katika utendaji. Pia aliwaomba wananchi watunze miradi iliyo kamilika ili idumu muda.
Akimkaribisha
Naibu waziri, Mheshimiwa Kasesela aliomba seriakli kuharakisha fedha
ili kukamilisha miradi ya maji na barabara, pia kuomba uwezekano kila
barabara zinapo jengwa yatengwe maeneo kwa ajili ya emergence unit ili
kuokoa miasha ya watu mara ajali zinapotokea. aliendelea " leo Mh waziri
umezindua maabara hapa Kising'a lakini eneo hili lipo barabara kuu ya
kuelekea Dodoma ajali zinapotokea tunapata tabu sana kuokoa maisha ya
wananchi ni muhimu sasa tanroads wana disign barabara mpya ziwepo pia
fedha za kujenga vituo vya dharura ambavyo vyawezwa kuunganishwa na
vituo vya kupumzikia wananchi ili halmashauri zetu zipumue mara
yatokeapo majanga".
Pia
akiongea kwenye mkutano wa watumishi Mkurugenzi wa halmashauri Bwana
Robert Munyusi pamoja na Katibu tawala wilaya ya Iringa Bwana robert
Chitinka wote kwa pamoja walimpongeza Naibu waziri kwa kasi kubwa ya
utendaji kazi wake.
Ziara
ilimalizika kwa kumtembelea Mwalimu aliye fiwa na mwanae wakati ziara
ikiendelea. Naibu waziri aliwafariji wafiwa na kutoa ubani kisha
kuendelea na safari kuelekea Dodoma.