BALOZI KARUME :CAMEROON HAJAPEVUKA KUTAWALA NA KIUONGOZI


Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Balozi Ali Abeid Karume amesema kujitoa kwa Uingereza katika Jumuiya ya Ilaya  (EU ) ni kutokana na udhaifu pia  kupwaya katika masuala ya uzoefu, uongozi na utawala ambako kumemtatiza Waziri Mkuu wake David Cameroon si vinginevyo.
Amesema kosa kubwa walililolifanya Waingereza ambalo watalijutia ni uamuzi wa kumkabidhi  madaraka ya juu ya  uWaziri mkuu mwanasiasa ambaye kihistoria  hajawahi hata kushika nyadhifa yoyote  nyeti ya kiserikali  huku akiwa mwanagenzi katika uwanja wa siasa na kwenye medani za kiutawala na diplomasia.
Balozi Karume ameeleza hayo jana katika mahojiano maalum na Raia Tanzania  yaliofanyika nyumbami kwake  huko Maisara Suleiman mjini unguja baada ya kuitishwa  kura ya maoni huko UK na Taifa hilo kujitoa katika umoja huo.
Balozi Karume alisisitiza kuwa Cameroon ameonyesha udhaifu na kukosa kabisa msimamo thabit hatimaye  akakubali kuyumbishwa kirahisi na kijikuta akiridhia kuiitisha kura ya maoni wakati Waingereza tayari walishakichagua  Conservertive anachokiongiza ambacho kilinadi  sera yake ya  kubaki katika EU katika uchaguzi ulokiweka madarskani huku vyama vingine vikipinga sera hiyo  .
Aliongeza kusema kwamba kama Cameroon  angelikuwa ni mweledi, mahiri na mjuzi wa kupanga karata za kisiasa, hakupaswa kuitisha kura ya maoni ambayo imeifanya nchi hiyo  ifikie maamuzi ya kujitos katika umoja huo ulioanziswa tokea  mwaka 1956 chini ya makataba ulioitwa "Roma Treat "
"Si lazima katika kutengeneza sera za nchi kila kitu waulizwe wananchi, maamuzi ya kiutawala na hata ya kikatiba yanaweza kuteezwa na chombo husika kwa niaba ya wananchi  , Conservative kilishatangaza msimamo wake wa kuwa mwanachama wa  EU, Labour na vingine  vikakataa , wananchi wa UK kwa hiari  yao wakakichagua conservative , ni dhahir waliziafiki sera hiyo hivyo hapakuwa na haja wala sababu ya msingi  kubadili msimamo"alisema
Aidha Balozi Karume alisisitiza huku  akishauri kuwa ni vyema nchi  katika  dhamira ya kuwakabidhi madaraka ya juu viongozi wake kwanza yakazingatiwa masuala mtambuka  yanayohusu  elimu,  weledi, uzoefu , ukomavu na upeo badala ya kubakabaka viongozi kwa bahati nasibu.
Alieleza kuwa pamoja na matokeo ya kura ya maoni kutaka England ijitoe,  nchi nyingine zinazounda The Great Britain zinahitaji kubaki katika umoja huo jambo ambalo linaoonyesha wazi kama Cameroon aliandamwa na kiherehere.
Balozi Karume akisisitiza zaidi, alisema hata mgombea urais wa Democratic huko Marekani Hillary Clinton amewahi kuelezea katika moja ya mikutano yake ya kampeni  juu ya umuhmu na haja ya mataifa kupata viongozi ambao wamebobea na kupevuka katika medani za uongozi , utawala na masuala anuai  yanayohusu upambanuaji na upambanuzi  wa masuala ya kidiplomasia kwa mapana stahili.
"Dhamana ya uongozi mzuri inahitaji pia ushupavu, kiuongozi mhusika lazima awe anayejiamini , kwasababu taratibu za kuongoza zinajitaji indahr,  umakini na maarifa mapana  "alisisitiza Balozi huyo mstaafu.
Akizungumzia kujitoa kwa UK katika EU alisema kwamba anachoamini ni kwamba waingereza wamekwepa na kukimbia  jukumu la kubeba gharama ya kuchangia kiasi kikubwa cha michango  na si kwasabahu ya tisho la  kuyumba kwa uchumi wake .
"Yaonyesha fika toka awali UK haikuwa na nia njema katika kujiunga kwake EU , waliingia na sharti la kukataa matumizi ya sarafu ya pamoja moja huku wakihimiza vinginevyo ili washiriki  fedha ya Uropa iwe na picha ya malkia wa Uingereza "Alieleza  Balozi Karume.
Pia  alisema hata utabiri wa aliyekuwa  Rais wa Ufaransa Charls DeGaulled mwaka 1973 wakati Uingereza  ikiomba uanachama katika EU A aliwahi kuwaasa wenzake  akitaka Uingereza isiruhusiwe kuwa mwanachama akilipigia Taifa hilo huku Balozi Karume  akisema utabiri huo sasa umetimia na kudhihirika.
Alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu aina ya muundo wa EU  kama ni imara zaidi huku  baadhi ya wanasiasa nchini wakifikia  hatua ya kuupigia debe uwe ndiyo mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar , Balozi huyo alisema wanasiasa  waliotaka muundo huo  walikuwa wakipigamia mfumo wa serikali tatu kwa malengo maalum  huku wakiamini kuwepo kwa marais watatu wasingefika mahali popote katika kuendesha serikali tatu zenye malengo , mipango na sera tofauti.
"Walitaka kupenya kupitia mlango wa serikali tatu ambazo walijua hazitaishi wala kusikilizana, matarajio yao izuke  mitafaruku ambayo ungepelekea kuvunjika kwa  muungano na kulisambatarika Taifa "alieleza Balozi Karume ambaye ni mtoto wa pili wa  Rais  wa kwanza Aanzibar Mzee Abeid Karume.
Hata hivyo alieleza kuwa pamoja na UK kijiondoa rasmi katika EU   anaamini mataifa megine yakiwemo Hispania, Greece na Ureno hayawezi kufikiria kijitow badala yake yataendelea kubaki katika umoja huo na kwamba  hautatetereka .
"Tuliwaelimisha  wanasiasa waliotaka Tanzania iige  muundo wa EU uwe ndiyo wa Jamhuri ya Muungano wa Tananzia, mapema kabisa niliwaeleza  EU ni ushirika wa kimaendeleo ya uchumi si muungano  ya kidola kama ilivyo UK , USA na haufai kuigwa na Tanzania "alisema Bakozi huyo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post