Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mipango wa Chama c ha Wananchi (CUF ) Omar Ali Sheikh anayesakwa na Polisi amesema hajapata wito rasmi wa jeshi hilo na kueleza si kweli kama amekimbilia shimoni nchini Somalia kwa kuhofia kukamatwa na kufikishwa mahakamani.
Amesema kinachofanywa na polisi Zanzibar ni muendelezo wa vitendo vya unyanyasaji, vitisho na ukamadamizaji wa haki dhidi ya viongozi wa CUF na wamachama wake .
Sheikh ameleeza hayo jana alipopigiwa simu na Raia Tanzania kufuatia taarifa ya polisi na kuandikwa kwenye vyombo vya habari kiongozi huyo anasakwa kwa udi na uvumba hivyo ajisalimishe.
Mkurugenzi huyo wa cuf alisema amesikia taarifa hiyo kupitia magazeti na kwamba hajapata wito wa jeshi hilo mara atakapotakiwa atakwenda kwa miguu yake mahali popote.
Alipoulizwa anadhani anaitwa na polisi kwa tuhuma ipi alisema huenda wanamwita kwasababu ya kumhusisha na matukio ya watu kukatiwa mazao yao mashambani kisiwqni pemba.
"Naieleza dunia hali ya amani Zanzibar iko mahaki pabaya, vitendo vya manyanyaso, ukamdamizaji na maonevu ni kinyume na haki za binadamu "Alisema sheikh.
Aidha alipotakiwa kueleza iwapo vitendo vya ukataji mazao, ushawishi watu kubaguana na kutozikana vilivyochomoza huko Pemba hufanywa kwa ushawishi wa voongozi wa cuf ili kutaka iundwe serikali ya mpito, alisema si kweli na kama chama chake kingetaka kiwemo katika smz kingekubali kushiriki uchaguzi wa marudiao machi 20 mwaka huu .
Sheikh alisisitiza kuwa hali ya kisiasa na usakamani tete huku vitendo vya maonevu na watu kupigwa husasan katika kisiwa cha Pemba vikiongezeka siku had siku na kuwafanya wananchi waishi kwa hofu.
"Siwezi kuikimbia nchi yangu na kujificha somalia au Kenya kama inaavyoelezwa , nimezaliwa zanzibar, nitakufa na kuzikwa hapa, katu sitaacha kupigania haki yetu iliodhulumiwa " alieleza .
Naibu Kamishna wa Makosa ya jinai na upelelezi Zanzibar DCI salum msangi amesema polisi inamsaka Sheikh na kwamba anakabiliwa na tuhuma za viitenndo kadhaa vyo uchochezi kisiwani humo.
DCI Msangi alisema tayari polo's imemkaamta aliytekuwa Mwakikishi jumbo la kiwani kwa tiketi ya cuf Hija Hassan Hijja na sasa yuko chini ya mikono ya polisi.
"Tunamsaka Sheikh na tunaamini tutamkamata, tayari mtu mmoja Hija Hassan Hija aliyekuwa akitatafutwa pamoja na sheikh tumpeta , tunaye kwa mahojiano "alisema .
Hata hivyo alisema si kweli kama kuna hali tete huko Pemba kama inavyoenezwa na baadhi ya watu kwa lengo la kutaka kuionyesha dunia kama hali si shwari au kumekithiri maonevu.
"Kama hali ni tete ikiwakabili wahalifu na pemba hakukaliki hilo ni kweli, temejipanga hasa kukomesha aina yoyotr ya vitisho na hujuma yeyote"alieleza