KASESELA:RASILIMALI KUBWA KULIKO ZOTE NI BINADAMU

Mkuu wa wilaya ya Iringa akiwa anafungua konga mano hilo 

Mkuu wa wilaya akipokea kitabu toka kwa bwana Daniel El Noshokaty ambaye alikabidhi vitabu kwa kila mwananfunzi kwa ajili ya kujisomea

 MKUU wa wilaya ya Iringa amefungua kongamano la Wanafunzi wa shule za sekondari kujadili Maendeleo na matumizi ya rasilimali.

 Kongamano hilo liliandaliwa na umoja wawalimu wa masomo ya Uraia CETA wakishirikiana na na KAS -taasisi ya kujerumani.

 Akifunga kongamano hilo mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisistiza kuwa rasilimali kubwa inayotakiwa kufanyiwa kazi ni Binadamu.

 Alisema kuwa binadamu akijengewa uwezo anaweza kubadilisha rasilimali hizi ziwe na faida kwa maisha yake na wengine. 


Aidha alisema kuwa suala la nidhamu kama msingi wa maisha, upendo na udailifu vinalete mabadiliko katika maisha ya mwanadamu.

 Naye Mwakilishi wa KAS bwana Daniel El Noshokaty akimkaribisha Mkuu wa wilaya alisema Taasisi ya KAS imeanza toka mwaka 1964 ikiwa na kazi ya kuelimisha wananchi juu ya elimu ya uraia hapa Tanzania na imetoa vitabu vingi kuhakikisha watanzania wanapata uelewa wa elimu hiyo.


 Kwa Irimga wataendelea kuelimisha wanafunzi watambue fursa zilizopo katika rasilimali nyingi. 

Kingamano hilo la siku moja lilikuwana na mada zenye kutambua uwezo wa nchi katika kuleta thamani kwa rasilimali zilizopo Tanzania hasusan Iringa. Shule za Lugalo, St Joseph, Kleruu, Kwelu, Highland na Mkwawa zililishirki katika kongamno hilo
wananfunzi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya (hayupo pichani)

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post