MUME ASHITAKIWA KWA KUMLAWITI MKE WAKE AKIWA MJAMZITO


Mkazi wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Jaribu Obedi (26) amehukumiwa
kifungo cha miaka 60 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuingilia kinyume
na maumbile mkewe.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya hiyo, Erick Marley alisema Mahakama
imeridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ambao bila ya kuacha
shaka umethibitisha mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo.
Alisema ametoa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwake na wanaume wengine
wanaokusudia kutenda kosa kama hilo.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Peter Makala alidai kuwa mshtakiwa huyo
alitenda kosa hilo kati ya Mei 28 na 30 usiku katika Kijiji cha Kumuhama.
Alidai mshtakiwa huyo alimfanyia kitendo hicho mkewe huyo kwa siku tatu
mfululizo wakati akiwa na mimba ya miezi saba.

Alidai kitendo hicho kilimuathiri kiafya na kukosa uvumilivu, hivyo kutoroka na
kwenda kutoa taarifa kwa dada yake anayeishi Mtaa wa Migombani mjini
Kibondo.

Mwendesha mashtaka huyo alidai baada ya dada yake kupata taarifa hizo,
alimpeleka katika ofisi za ustawi wa jamii kisha polisi na ambako alipewa fomu
namba tatu PF3 ili kwenda kutibiwa hospitali.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post