No title

WAJASIRIAMALI 120 kutoka mitaa ya jiji la arusha wamenufaika bure na elimu ya mlipa kodi lengo likiwa ni kuwaingiza kwenye mfumo wa ulipaji kodi bila shuruti.

Akizungumza katika semina hiyo iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali inayoshughulikia mambo ya kijamii Gola faundition,Mkurugenzi wa taasis hiyo Salawe Magembe alisema kuwa wameamua kutoa semina hiyo ili wajasiriamali waelewe umuhimu wa kulipa kodi.

Alisema kuwa wajasiriamali hawajui umuhimu wa wao kulipa kodi na hivyo kupitia elimu wanayoitoa itakuwa chachu ya kuwafanya watambue wajibu wao wa ulipaji kodi bila kulazimishwa.

"Tulichogundua kwa hawa wajasiriamali ni kwamba wanakabiliwa na elimu ya uelewa juu ya kulipa kodi wanajua wanaolazimika kulipa kodi ni wafanyabiashara wakubwa tu hali ambayo inachangaia hata kutopatikana kwa maendeleo kwani hawajui kuwa hizi kodi ndio zinaboresha maendeleo yao"alisema Salawe.

Aidh alieleza umuhimu wa wajasiriamali kulipa kodi kiwa ni pamoja na kuwa na haki ya kudai elimu bora,miundombinu lakini pia kuwawezesha kunufaika na ruzuku ya serikali kuu.

Aliwataka wajasiriamali kutumia fursa walizo nazo za kibiashara za kuchangia pato kwa kupitia ulipaji kodi ili waweze kutatuliwa changamoto zinazowakabil.

Mmoja wa washiriki wa semina hiyo ambaye mwenyekiti wa kijiji cha eng"ida group Ruth Msuya alisema kuwa sio wajasiriamali wote wanaelewa umuhimu wa ulipaji kodi na hivyo elimu waliyoipata imewasaidia kuelewa wajibu wao wao na kwamba swala la ulipaji kodi ni la kila mtu na sio la ukwepaji

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post