Mkurugenzi Mtendaji wa
shirika lisilo la kiserikali la Haki Ardhi Yelfred Mienzi akiendelea kutoa kutoa mada katika mkutano huo
wajumbe wakifuatilia mada zinazoendelea
mmoja wa washiriki akichangia mada katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa lush garden jijini hapa
Na Woinde Shizza, Arusha
Wadau wa masuala ya ardhi kutoka taasisi zisizo za
kiserikali wamesema mchakato unaoendelea hivi sasa wa kuainisha
mapendekezo ya mabadiliko ya sera ya ardhi nchini unapaswa kutumika
vizuri kwa wadau wote kwa kutoa maoni yatakayosaidia kupata sera
iliyobora ili kuondoa migogoro ya ardhi iliyokithiri katika maeneo yote
nchini.
Wadau hao wamesema hayo jijini hapa katika mkutano
uliowakutanisha wataalamu kutoka Taasisi hizo kwa lengo la kupitia maoni
yaliyo tolewa na Taasisi zote za kiraiya na kupata mapendekezo ya
jumla yatakayowasilishwa serikali ni.
Wataalamu wa ardhi kutoka taasisi mbalimbali zisizo za
kiserikali nchini wamekutana jijini ARUSHA kwa lengo la kupitia maoni
yote yaliyoanishwa na Taasisi hizo ili waweze kupata mapendekezo ya
jumla yatakayo wasilishwa serikalini kwa lengo la kuboresha sera ya
ardhi.
Wamesema kuwa bado jamii haijashiriki vya kutosha
kulingana na matizo yaliyopo, ambapo ni vema wadau wote wakatumia
nafasi iliyotolewa na serikali kutoa maoni yao ya kutosha juu ya sera
hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa
shirika lisilo la kiserikali la Haki Ardhi Yelfred Mienzi alisema kuwa
zipo changamoto nyingi katika masuala ya ardhi zinazohitaji jamii
kushiriki kwa mapana kutoa mawazo yao ili waweze kuisaidia serikali
kutoa sera itakayotatua migogoro iliyokithiri katika maeneo mbalimbali
nchini haswa vijijini na mjini.
"unajua hii ni fursa ya wananchi kutoa maeneo yao juu ya
sera hii ya ardhi kama m navyosumbuliwa ardhi ni kila kitu sasa iwapo
tunatatoa maoni yetu Vibaya sisi ndio tutakuwa, unajua aya maoni yetu
yakupelekwa ndio yanatengeneza sera sasa sera inaweza kuwa nzuri kwetu
iwapo itakuwa nzuri na itakuwa mbaya kwetu iwapo tutaboronga"alisema
Mienzi.
Naye Mwakilishi kutoka chama cha wanasheria wanaotetea haki
za Wanawake Tanzania, Naseku Kisambu alisema kuna umuhimu wa kuipitia
sheria ya ardhi kwa kina ili iweze kutoa haki kwa Wanawake hasa katika
umiliki wa ardhi kutokana na wao kunyimwa haki kwa muda mrefu sasa.
Alisema kuwa katika sheria ya ardhi iliopita amna sehemu
inapoainisha kuwa mtoto wa kike anaweza kupewa umiliki Shi wa ardhi,
hivyo nivigumu mwanamke kumiliki ardhi labda ukute kazawadi wa au
kununua mwenyewe hivyo watatumia fursa hii ya kuchangia sera hii ili
kutoa mapendekezo ya kusaidia mwanamke kumiliki au kumilikishwa ardhi.
Gazeti hili liliongea na Mkurugenzi mtendaji wa chama cha
Waandishi wa habari za mazingira Tanzania John Chakomo naye alisema ni
vizuri makundi yote yanayotoa maoni yao, yakatoa mapendekezo
yatakayoifaidisha jamii yote bila kupendelea makundi yao wanayoyatetea.
Alisema kuwa iwapo haki na sheria ikifuatwa ya kukusanya maoni basi itasaidia kupata sera nzuri itakayo mlenga kila mwananchi.
Kwa upande wake Mwakilishi wa taasisi ya CARE, Mery Ndalu,
amesema tayari asasi mbalimbali wameshatoa maoni yao ambapo mkutano huo
umeyapitia na sio kupitia tu basi watayaboresha ili waweze kutoa
mapendekezo yatakayoisaidia serikali kutengeneza sera itakayoleta tija
kwa wananchi.
Aidha alisema kuwa wanatarajia kupeleka mapendekezo
yatakayosaidia kuboresha haki za umiliki ardhi wa kimila ili kutoa fursa
kwa jamii ya watu wachini kufaidika na ardhi yao.
Mwakilishi kutoka chama cha wanasheria wanaotetea haki
za Wanawake Tanzania, Naseku Kisambu akieleza kwa ufupi jinsi chama chao walivyojipanga kusaidia wanawake katika sera hii ya ardhi