Meneja wa Uber Kusini mwa Sahara, Alon Lits akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa jukwaa la mtandao ubunifu wa kiteknolojia la Uber.
Baadhi ya waanzilishi na wadau usafiri wa Uber wakiwa katika uzinduzi usafiri wa uber jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wakiwa katika uzinduzi wa usafiri wa uber jijini Dar es Salaam leo.
JUKWAA la mtandao ubunifu wa kiteknolojia la Uber lazindua usafiri wa Uber jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la urahisisha usafiri kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja wa Uber Kusini mwa Sahara, Alon Lits amesema kuwa jukwaa
la ubunifu wa kiteknolojia, Dar es Salaam inaungana na orodha ya vituo
maarufu vya usafiri barani Afrika, mafanikio ya Uber katika nchi nyingi
imeshazinduliwa na kuwa na mafanikio makubwa.
“Tunajivunia
kuzindua Uber nchini Tanzania katika muda ambao uchumi wake unakua.
Wakati miundo mbinu ya Dar es Salaam ikiwezeshwa kuwa ya viwanda, hivyo
huongezeka kwa mahitaji ya usafiri nafuu, rahisi na wa
kuaminika.”Amesema Lits.
Lits amesema kuwa kwa kutumia usafiri huo
wasafiri
watasafiri kwa muda muafaka ukiwa na program ya maombi ya
usafiri(Application), kwa kubonyeza tu kitufe ambacho kitatoa taarifa
kwa dereva aliyepo karibu pia amesema kuwa Uber husaidia
watu kupata usafiri kwa kubonyeza tu kitufe pia hakuna kusubiri
barabarani au kutembea maeneo jirani usiyoyajua kwa ajili kutafuta
basi.
Amesema kuwa hakuna haja kusimamisha gari mtaani au kuwa nje kusubiri
usafiri. Kwa usalama zaidi utaweza kutumia App ya Uber mahali ulipo
ukisubiri gari ifike. Hii ikimaanisha hakuna haja ya kusimama barabarani
kusubiri taksi au kuhangaika kutafuta kituo cha basi kilicho karibu
muda wa usiku.
Safari hazina kificho mara dereva anapokubali ombia lako, unaona jina
lake la kwanza, picha na namba ya gari yake. Pia unaweza kuangalia kama
kuna abiria wengine waliofurahia huduma yake. Kwa kuongezea, dereva
anaweza kuona jina lako la kwanza na alama ulizompa. Unaweza kuwasiliana
na dereva, naye pia akawasiliana nawe-kupitia hii App kama kuna
mkanganyiko wowote kuhusu muda wa kukuchukua.
“Uber
ni sehemu ya mageuzi makubwa duniani katika Nyanja ya usafirishaji. Dar
es Salaam ipo juu, inazizima, mji unaokuwa ukiwa na vijana mahiri wenye
nguvu ya kufanya kazi ambao wapo tayari kutukaribisha na kusapoti huduma
yetu. Pamoja, kwa ushirikiano na mipango ya usafiri iliyopo jijini Dar
es Salaam tunaweza kubadilisha sura ya usaifiri wa mjini kunufaisha
abiria. Tuna furaha isiyo na kifani kwa uzinduzi huu.”amesema.