DAR ES SALAAM inakuwa mji wa 475 kujiunga na mtandao unaokuwa wa
Uber duniani. Kwa uzinduzi wa Uber, jukwaa la ubunifu wa kiteknolojia, Dar
es Salaam inaungana na orodha ya vituo maarufu vya usafiri barani Afrika.
Kufuatia mafanikio ya Uber katika nchi nyingi, Uber inayo furaha kuzindua
jukwa la ushirika la abiria kwa watu wa Dar es Salaam.
Jukwaa la mtandao wa ubunifu la Uber, huwaunganisha madereva na
wasafiri kwa muda muafaka, kwa kubonyeza tu kitufe. Au ukiwa unatoka
na marafiki kwenda mjini kibiashara, au kuangalia vivutio vya kitalii, Uber
hutoa njia rahisi yenye unafuu kufika kila mahali.
Dar es Salaam Jiji linalokua kwa kasi kibiashara, linafanya iwe ni mahali
sahihi kwa Uber. Taarifa za Benki ya Dunia zinasema kwamba Pato halisi
la Tanzania (GDP) linakadiriwa kuwa 6.8% kwa mwaka 2017 na nchi
imeweza kuhimili mfumuko wa bei. Biashara zinakua kwa kasi katika sekta
za usafiri, ujenzi na fedha.
Meneja wa Uber Kusini mwa Sahara, Alon Lits anasema: “Tunajivunia
kuzindua Uber nchini Tanzania katika muda ambao uchumi wake unakua.
Wakati miundo mbinu ya Dar es Salaam ikiwezeshwa kuwa ya viwanda,
hivyo huongezeka kwa mahitaji ya usafiri nafuu, rahisi na wa kuaminika.”
Akaongeza, “Tumeweka viwango vya kuunganisha watu katika usafiri
wenye kiwango cha juu duniani, kusafirisha mamilioni ya watu duniani kote
kila siku kupitia huduma zetu za usafiri nafuu na za kuaminika kwa
kubonyeza kitufe tu. Huduma zetu zinaenda sambamba na aina za usafiri
uliopo, hivyo wote tunaweza kufanya kazi pamoja kupunguza foleni
barabarani na kuboresha mazingira ya usafiri katika jiji.
Kwanini Uber?
Uber husaidia watu kupata usafiri kwa kubonyeza tu kitufe-hakuna kusubiri
barabarani au kutembea maeneo jirani usiyoyajua kwa ajili kutafuta basi.
Ni njia bora na karibu zaidi kupata usafiri salama, nafuu na wa kuaminika.
Kabla ya kuingia ndani ya gari
Hakuna haja kusimamisha gari mtaani au kuwa nje kusubiri usafiri. Kwa
usalama zaidi utaweza kutumia App ya Uber mahali ulipo ukisubiri gari
ifike. Hii ikimaanisha hakuna haja ya kusimama barabarani kusubiri taksi
au kuhangaika kutafuta kituo cha basi kilicho karibu muda wa usiku.
Safari hazina kificho. Mara dereva anapokubali ombia lako, unaona jina
lake la kwanza, picha na namba ya gari yake. Pia unaweza kuangalia
kama kuna abiria wengine waliofurahia huduma yake. Kwa kuongezea,
dereva anaweza kuona jina lako la kwanza na alama ulizompa. Unaweza
kuwasiliana na dereva, naye pia akawasiliana nawe-kupitia hii App kama
kuna mkanganyiko wowote kuhusu muda wa kukuchukua.
Wakati wa Safari Julisha mahali ulipo.
Unaweza kuwajulisha ndugu na marafiki zako kwa
furaha zaidi juu ya mipango ya safari yako kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na
mahali ulipo, na muda unaotarajia kuwasili. Watapokea linki ambapo
wataweza kuona muda kamili, jina na picha ya dereva, gari lake na mahali
ulipo katika ramani hadi utakapowasili na wanaweza kufanya haya yote
bila haja ya kupakua App ya Uber wao wenyewe.
Baada ya Safari
Fanya mrejesho na toa alama kila baada ya safari. Baada ya kila safari,
wewe na dereva wako mnahitaji kupeana alama na kufanya mrejesho.
Timu yetu ya usalama hupitia taarifa hizi na kufanya uchunguzi juu ya kila
jambo.
Msaada masaa 24 kwa wiki.
Endapo jambo litatokea ndani ya gari, kama ni ajali ya barabarani au
kutoelewana kati yako na dereva, mfanyakazi wetu wa huduma kwa wateja
yupo tayari kukusaidia kwa suala lolote masaa 24 kwa wiki. Msaada wa
Haraka. Tuna timu mahiri inayoshughulika na matukio kujibu suala lolote
linalohitaji ufumbuzi wa haraka. Tukipokea taarifa kuwa dereva au abiria
amesababisha tukio la hatari au hayupo njia sahihi, tunafunga akaunti zao
na kumzuia asiweze tena kuingia katika jukwaa la Uber wakati tukifanya
uchunguzi.
Nyuma ya Pazia
Muda wote kwenye ramani. Kukubali kuwajibika ni moja ya mambo
yanayofanya wasafiri kujisikia wako salama ndani ya Uber. Tunatumia
teknolojia ya mawasiliano ya GPS kuweka taarifa za mahali madereva
wanakotakiwa kwenda wakati wa safari, ili kutuwezesha kuthibitisha njia
zinazotumika ni bora, kitu kichanachojenga uwajibikaji na ushawishi
mkubwa kwa utendaji mzuri.
Utendaji na mamlaka za sheria. Endapo mamlaka za kisheria zinatupa
taratibu za kisheria, tunatafanya kazi kutafuta vielelezo, mfano kwa kutoa
taarifa za safari. Hata hivyo uwazi na uwajibikaji upo katikati ya mafanikio
ya Uber. Upimwaji wa madereva. Madereva wote lazma awapitie mchakato
wa upimwaji kabla ya kuanza kutumia App ya Uber
Alon Lits aliongeza: “Uber ni sehemu ya mageuzi makubwa duniani katika
Nyanja ya usafirishaji. Dar es Salaam ipo juu, inazizima, mji unaokuwa
ukiwa na vijana mahiri wenye nguvu ya kufanya kazi ambao wapo tayari
kutukaribisha na kusapoti huduma yetu. Pamoja, kwa ushirikiano na
mipango ya usafiri iliyopo jijini Dar es Salaam tunaweza kubadilisha sura
ya usaifiri wa mjini kunufaisha abiria. Tuna furaha isiyo na kifani kwa
uzinduzi huu.”
Uber inasherehekea uzinduzi mjini Dar es Salaam kwa kutoa huduma ya
bure ya usafiri. Tanzania wanaweza kujaribu huduma mpya kwa kupata
huduma ya bure kwa kuingia kwenye App ya Uber.
MAKUBALIANO (vigezo kwa usafiri wa bure)
Ni lazima upakue App ya Uber na weka kificho cha promosheni
MoveTanzania ili upokee usafiri wa bure
Usafiri wa bure utapatikana kutoka Alhamisi Juni 16 saa 6 mchana mpaka
Jumapili Juni 19 katikati ya usiku.
Watumiaji watapata usafiri wa bure kwa safari sita tu na kila safari isizidi
kiasi cha shs 12,000
Usafiri wa bure utapatikana tu kwa safari zinazoanzia na kuishia maeneo
ya Dar es Salaam yaliyopangwa.