Na Woinde Shizza,Arusha
WANANCHI 43
wakazi wa eneo la Mianzini, Timbulo wilayani Arumeru mkoani Arusha,wamemwomba
Rais John Pombe Magufuli kuingilia kati Mgogoro dhidi yao na Halmashauri ya Arusha kufuatia Halmashauri
hiyo kukaidi hukumu ya mahakama iliyo elekeza wananchi hao kulipwa fidia katika
upanuzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 8.
Wakizungumza
na vyombo vya habari jana moja ya wananchi hao, Fanuel Lamai na wenzake sita walio
fungua kesi , kwa niaba ya wananchi hao alisema kuwa mwaka 2013 walifungua kesi
ya ardhi namba 18 katika mahakama kuu mkoani Arusha dhidi ya halmashauri ya
Arusha wakipinga hatua ya kubomolewa nyumba zao bila kulipwa fidia katika mradi
wa upanuzi wa barabara ya Mianzini Timbulo unaotekelezwa na halmashauri ya Arusha.
.
Alisema kuwa
bara bara hiyo ambapo hapo awali upanuzi wake ulitakiwa kuwa mita 10 kwa 10
wananchi hao walipinga na kueleza mahakama kuwa bara bara hiyo haikuwepo wakati
wananchi hao wana anzisha makazi kwani kipindi hicho eneo hilo lilikuwa ni njia
ya mapito ya mifugo.
Katika hukumu
ya kesi hiyo iliyotolewa na Jaji Fatma Massengi wa mahakama kuu alielekeza upanuzi wa barabara hiyo ufanyike mita 4 kwa
4 badalaya ya mita 10 kwa 10 na ikasema ipo haja kwa halmashauri na wananchi
hao kukaa na kuridhiana iwapo itaongeza kiwango cha upanuzi hukumu ikielekeza
kuwa wananchi hao wanapaswa kuendelea kuishi kwenye ardhi yao .
Wananchi hao
wamesikitishwa na hatua ya halmashauri kuanza upanuzi wa barabra kwa kubomoa
nyumba zao zaidi ya 30 zilizofunjwa hadi sasa bila kujua iwapo watafidiwa kama
mahakama hilivyo elekeza.
Wananchi hao
wakiwemo wazee na wajane wamemwomba Rais Magufuli kuingilia mgogoro wao kwa kuiamuru
halmashauri isitishe zoezi la kuvunja nyumba zao hadi hapo watakapo patiwa fidia
wanazo dai zinazofikia kiasi cha shilingi bilioni 3.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha Lembris Noha alisema kuwa halmasahuri
hiyo aitalipa fidia kwa wananchi hao na
wanasimamia sheria ya ardhi ya mwaka 1932 inayo elekeza kuwa upanuzi wa bara
bara mita 10 kwa 10 auna fidia na kuwataka wananchi hao kusoma vizuri hiyo
hukumu na kuelewa na wasikurupuke kuwadanganya wenzao ambao wameelewa na kuanza
kubomoa wenyewe nyumbza zao .