Meneja wa bank ya CRDB tawi la Usa
River wilayani Arumeru mkoani arusha akimlisha keki moja ya mtoto alieshiriki
katika maadhimisho ya siku ya mtoto Africa iliyoandaliwa na bank hiyo katika
viwanja vya Usa River Academy.
Watoto wakishandana kukimbia katika siku
ya mtoto wa Africa iliyoandaliwa na bank ya CRDB tawi la Usa River wilaya ya Arumeru
mkoania Arusha katika viwanja vya usa river academy.
Watoto wakishandana kukimbiza kuku
katika michezo iliyoandaliwa na bank ya CRDB tawi la Usa River wilayani Arumeru
mkoani Arusha hivi karbuni katika michezo ya kuazimisha siku ya mtoto wa Africa
iliyofanyika katika viwanja vya shule ya Usa River Academy.
Watoto wakishandana kukimbia na magunia
katika siku ya mtoto wa Africa iliyoandaliwa na bank ya CRDB tawi la Usa River
wilaya ya Arumeru mkoania Arusha katika viwanja vya usa river academy
Na Woinde Shizza,Arusha
Benki ya CRDB tawi la Usariver
imewahimiza wazazi na walezi kujenga tabia ya kuwaendeleza watoto katika
michezo na vipaji walivyonavyo ili viweze kuwaimarisha kiakili na kimwili na
kuwanufaisha baadae.
Meneja wa Tawi hilo Jenipher
Tondi ameyasema hayo katika michezo ya watoto iliyoandaliwa na benki hiyo
katika viwanja vya USARIVER ACADEMY ambapo watoto walipata fursa ya kucheza
michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,netiboli,kukimbiza kuku na mbio za
kukimbiza magunia..
Amesema kuwa wazazi hawana budi
kuendeleza vipaji vya watoto kwani vinaweza kuwa na faida kwa familia,jamii na
taifa. “wazazi wawape watoto nafasi ya kushiriki katika michezo ili kuweza
kuvumbua vipaji vyao vilivyojificha sababu vipaji ni ajira tosha”
Pia amewakumbusha wazazi kuwawekea
watoto akiba ya fedha kwa ajili ya kumsaidia mtoto katika kulipa fedha za ada
kwa kufungulia account zisiszo kuwa na riba.
Kwa upande wao watoto walioshiriki
katika michezo hiyo Oscar Damian na Angela John wameishukuru benki hiyo kwa
kuwajali na kuwapa nafasi ya kukutana na watoto wenzao ambapo wameweza
kuburudika na michezo iliyoandaliwa.
Jane Nassari amewataka wazazi
kujenga utamaduni wa kuwaruhusu watoto wao kushiriki kwenye michezo kwasababu
michezo huleta afya ya akili,furaha na mashirikiano.
Mzazi aliyefika katika siku hiyo
Angelina Joseph amesema kuwa mazingira bora ya michezo yanapaswa kujengwa
ili watoto wapende michezo na kunufaika nayo kwa kuitumia kama njia ya
kujiimarisha kiafya na kiakili.