Na Woinde Shizza, Arusha
Umoja wa vijana wa chama Cha Mapinduzi umesema madai yalitolewa na mwanataaluma Jenerali Twaha Ulimwengu kutaka Mwenyekiti wa CCM na Rais mstaafu Dk jakaya Kikwete ashitakiwe mahakamani ni utoto na upuuzi mtupu kwani bado ana machungu ya kuambiwa ni Mnyarwanda si
Mtanzania
Pia anakuwa mbogo baada ya kufutika kwa matumaini yake kisiasa na sasa amejikuta kila wakati akiweweseka baada ya kuwekwa kapuni akisahauliwa na wenzake aliofanyakazi nao kwa muda mrefu akiwemo Mzee Benjamin mkapa na Dk Kikwete .
Hayo yametamkwa leo na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini hapa.
Sabaya alisema wakati Mkapa akiwania urais, Jenerali akajifanya mpambe wa mkono wa kulia ila kilichomshangaza na ambacho ni siri , Mkapa hakumtazama kwa jicho la huruma wala kumpa bashishi .
Alisema kuanzia hapo kalamu ya jeneraki katika uandishi wa makala zake za uchambuzi zikaindamana , kuinanga na kuisakama serikali ya Rais msaafu Mkapa kwa miaka yote kumi.
"Wakati fulani Mzee Mkapa katika moja ya majukwaa ya kitaaluma pale chuo kikuu cha Dar es salaam akamtolea uvivu baada ya kushindwa kumstahamilia na kujikuta akisema wapo ambao huandika kwa chuki dhidi ya serikali yake kila wiki kwasababu tu watu hao tumewanyima madaraka na vyeo" alisema Sabaya
Aidha Mweyekiti huyo wa uvccm alieleza kwa kipindi kirefu mwanataaluma na mwanasiasa huyo akaaamua kupotea kwenye ramani ya kisiasa na kuishi a kupambana na maneno ya serikali
Alisema wakati akihesabika ni kada shupavu wa wa CCM na mwaminifu toka akiwa kijana na kwasababu ambao ni zaidi ya uraia, usalama na hadhi ya kutopewa dhamana ya juu, hakuwa kama wenzake katika medani za kukabishiwa dhamana za utawala.
Sabaya alisisitiza kuwa aidha kwa yale ambayo Jenerali alikuwa akiyajua na asiyoyajua kwa makada wenzake na vyombo vya dola wakiwa wanajua kwa undani na ushahidi kwa kumjua zaidi ya anavyojijua,akajikuta akishindwa kufikia malengo yake kisiasa.
"Kiini cha kutopewa nyadhifa na madaraka ya uongozi kwa kadri alivyojiamini ai kutaraji hakuambulia lolote kwasababu hakuwa akitosha pia medani za utawala zilikuwa zikijua amepungukiwa sifa kadhaa muhimu na nyeti za kiongozi kipewa amana ya uongizi kwa kiwango alivyotaraji akabidhiwe"alieleza sabaya .
Mwenyekiti huyo akizungumzia madai ya mchakato wa uundwaji wa katiba mpya uliodaiwa na Jenwrali umeshindwa haukufikia tamati alisema madai ya Jenerali katika hoja hiyo alisema ndo ameonyesha kuchanganyikiwa kwasababu alichokieleza haskina ukwell na kwa hilo anafiiiri amekurupuka bila kujiandaa kihoja na kisailolojia .
"Si watawala wengi ambao huwa na fikra, ujasiri, mawazo au utamaduni wa kuzungumzia mabadiliko ya Katiba ya nchi zao hasa wanapokuwa madarakani hususan Barani Afrika , Dk Kikwete amethubutu , kuobyesha na kutenda , ni uamuzi ni wa aina yake uliowashamgaza viongozi na wanasiasa hata ndani ya CCM
"alieleza sabaya akisimsifu Dk Kikwete
Hata hivyo akieleza huku akikuvutiwabna maneno ya Dk kikwete , Sabaya alisema pale aliposema kwa kujiamini"midhali Taifa letu limefikisha miaka 50, ipo haja sasa ya kuandika upya Katiba yetu kulingana na mahitaji yaliopo pia matakwa ya wakati huu na ujao kwa miaka mingine 50 na zaidi"alieleza akinukuu matamshi ya Rais mstaafu Kikwete
Alisema UVCCM wanamtaka Jenerali aache kupotosha ukweli na kwamba mchakato wa katiba haujakwama ila umezingwa na miingiliano ya vipindi vya uuitishaji kura ya maoni , muda kioindi cha uchaguzi mkuu oktoba mwaka 2015 na muda wa kisheria kwa Rais aliyeanzisha mchakato huo kubaki madarakani kikatiba na kisheria.
Kwa upande wa matumizi akiyodai ni mabaya kwa fedha za umma , sabaya alisema idhini ya matumizi ya fedha hiyo ziliidhinishwa na bunge kwa nia na dhamira njema ya Taifa baada ya kuundwa kwa sheria ya mabadiliko ya katiba.
" kazi kubwa ya uandikaji wa Katiba imekamilika, rasimu ya Katiba imekabidhiwa serikalini, kinachotakiwa ni kuitishwa kura ya maoni ili wana nchi watumie haki yao kidemokraia kuamua kwa kusema ndiyo au hapana"alieleza.
Hata hivyo sabaya alisema alichokionyesha Jenerali mbele kadamnasi wakati akihudhuria kongamano pale chuo kikuu nibkejeli na dharau isiyostahili , ameonekana akiwa nabnyongo ya hamaki kutokana na kumbukumbu zile zile za kuwekwa kando ya utawala wa Mkapa kisha kuzikwa katika kaburi la sahau na utawala wa Dk Kikwete.
"Vyovyote vile iwavyo Dk Kikwete hawezi kushitakiwa kwa mujibu wa Katiba na sheria, hana shitaka linaloweza kumkabili kama anavyojaribu kuota njozi za mchana Jenerali na walio nyuma yake alisema .
Sabaya alisema UVCCM Mkoa wa Arusha tunawataka wananchi wema kumpuuza Jenerali kwasababu anaelekea kuzeeka vibaya huku akiwa majerahabya hamaki na hasira za mkizi.
Pia UVCCM wangeomba mtu huyo apuuzwe na wala wananchi wasikubali kunasa mtegoni kwa ushawishi wa maneno yake ya kupika ambayo yamejaa ghiliba na hadaa huku Jenerali akipania kusaka umaarufu mpya usioweza kumpatia tija wala faida .
"Tulitegemea sana Jenerali atamke na kutaka Dk Kikwete ashitakiwe mahakamani kwa kutumia fedha za umma katika ujenzi wa shule za msingi, sekondari, zahanati ,vyuo, barabara za lami, madaraja na majengo ambayo hayakuwepo tokea enzi za wakoloni hadi kuanza kwa utawala wa awamu ya kwanza "alisisitiza
Sabaya anaeleza kuwa UVCCM imepania kumfundisha na kumuelisha Jenerali kilabatakapoteleza ilivaache kukurupuka na kueneza maneno yabuongo hukubakikamusha kuwa si kama CCM ilihofia na haikutaka ujio wa vyama au Mwalimu Nyerere ndiye aliyeshinikiza kuingia kwa mfumo huo.
Alisema Tume ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko ya mfumo wa kisiasa ilioongozwa na Marehamu Jaji Francis Nayalali ambayo iliundwa na Mzee Mwinyi wakati akiwa Rais.
Kadhalika UVCCM Mkoa wa Arusha inalaani vikali matamshi ya upotoshaji yaliofanywa na Jenerali ambaye anaonekana bado anaugulia vidonda vyab kisiasa baada ya matarajio na ndoto zake kuvia na kwenda kombo.