Mbunge wa Ngorongoro Wiliam Olenashak.
Serikali
imesema itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kikamilifu katika
kuendeleza na kukuza uchumi wa nchi kwa sekta ya kilimo ikiwemo
kuendelea kuziboresha miongozo.
Akizungumza
kwenye ufunguzi wa mkutano wa wazalishaji wa mbegu ndani na nje kutoka
katika makampuni mbalimbali ya mbegu Naibu waziri wa kilimo,uvuvi na
mifugo Wiliam Olenash amesema lengo la kuzindua mfumo huo ni ili
kuboresha zaidi katika sekta ya kilimo.
Mh.Olenash
amesema serikali wanatambua mchango unaopatikana kutoka sekta binafsi
hivyo watahakikisha maslahi ya wadau ikiwemo makampuni binafsi na
wakulima yanapewa kipaumbele na kulindwa.
Pia
amezitaka Taasis za uzalishaji wa mbegu kushughulika na upatikani wa
mbegu bora zilizo na tija kuweza kuongeza uzalishaji ili kuleta
maendeleo kwa wakulima.
Aidha
licha ya kuwepo kwa ugonjwa wa mahindi ambao umepelekea kuathiri kwa
kiasi kikubwa uzalishaji wa zao hilo na kusababisha kuzorota kwa ukuaji
usioridhisha.
Amesema
kuwepo kwa changamoto ya upungufu wa wataalam wa kilimo ,elimu
isiyotosheleza juu ya matumizi sahihi ya kanuni kilimo pamoja na
wataalam hivyo serikali imeahidi kuendelea kukabiliana na changamoto
hizo.