Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John
Magufuli akikabidhi tuzo kwa mshindi wa kwanza wa Tuzo ya Rais ya mzalishaji bora
wa mwaka 2015, kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin wakati wa hafla ya kutoa tuzo kwa washindi iliyofanyika jijini katika
hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam . Wengine ni Mwenyekiti wa Chama Cha
Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Dk. Samwel Nyantahe ( wa pili kulia) na
kushoto ni Waziri wa Biashara ,Viwanda na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage.
Mkurugenzi Mkuu wa
TBL Group na maofisa waandamizi wa kampuni wakifuatilia matukio wakati wa hafla
hiyo
Rais John Magufuli
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha wafanyabiashara wenye
viwanda na watendaji wa makampuni ambayo yameshinda tuzo mbalimbali katika
kipindi cha mwaka huu
Mkurugenzi Mkuu wa TBL
Group,Roberto Jarrin (wa nne mstari wa mbele kutoka kushoto) akiwa katika picha
ya pamoja na maafisa wa kampuni hiyo waliohudhuria hafla ya kukabidhiwa tuzo
Kampuni
ya TBL Group imeibuka mshindi wa kwanza
wa tuzo ya Rais ya mzalishaji bora kwa kipindi cha mwaka 2015,vilevile imeibuka
mshindi wa kwanza katika kundi la uzalishaji wa vinywaji ambapo imetunukiwa tuzo kwa ushindi huo.
Tuzo ya
mzalishaji bora hutolewa na Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI na hafla
ya kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali imefanyika leo jijini Dar es salaam
katika hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam ambapo mgeni wa heshima aliyekabidhi tuzo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa John Magufuli.
Akiongea
baada ya hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa
TBL Group,Roberto Jarrin,alisema ushindi huu ni zawadi kwa wafanyakazi wote wa
kampuni kwa kuwa jitihada za kila mmoja
ndizo zimepelekea mafanikio haya kupatikana.
“Kwetu
TBL Grop tunayo furaha kwa kushinda tuzo hizi tulizofanikiwa kuzinyakua siku ya
leo,haya kwetu ni mafanikio makubwa na tumefurahi kuona mchango wa uwekezaji
wetu unatambuliwa na tunaendelea kuwa washindi wa tuzo mbalimbali zinazotolewa
na taasisi mbalimbali”.Alisema Jarrin.
Alisema
TBL Group itaendelea kufanya uwekezaji zaidi nchini na kuchangia kukua kwa
uchumi wa taifa ikiwemo kuunga mkono jitihada za serikali za kupunguza tatizo
la ajira nchini ambapo mbali na kutoa ajira kwenye viwanda vyake na mtandao wa
wafanyabiashara inaoshirikiana nao tayari imeanzisha miradi ya kuwasaidia
wakulima ambayo tayari imeanza kuonyesha mafanikio kwa kubadilisha maisha ya
wakulima kuwa bora.
“Tunaishukuru
serikali ya Tanzania kwa kufanya kazi kwa karibu na wawekezaji na nina imani
tutaendelea kushirikiana ili kuweza kupata mafanikio zaidi katika siku za usoni”.Alisema.