SEREKALI YATAKIWA KUANGALIA KWA MAKINI BAJETI YAO YA MWAKA WA FEDHA 2016/2017 KWA KUANGALIA ZAIDI SEKTA YA AFYA PAMOJA NA ELIMU


Na Woinde Shizza,Arusha
BAADHI ya wananchi wa mkoani Arusha wameiomba serikali kuhakikisha
bajeti ijayo ya mwaka wa fedha inawaangalia kwa jicho la pili wananchi
wenye kipato cha chini ambao hawana uwezo wa kukidhi baadhi ya
mahitaji yao kwa kupunguza bei ya bidhaa ili kupunguza makali ya
maisha

 Serikali ya awamu ya tano kama  itaweza kupunguza baadhi ya
kodi katika mahitaji muhimu basi maisha ya wananchi wenye kipato cha
chini yataweza kuboreka na hivyo umaskini utapungua kwa kiwango
kikubwa tofauti na sasa.

Hayo yameelezwa na wananchi wa jiji la Arusha wakati wakiongea na
  Na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na bajeti ijayo ya serikali ambapo wamedai
bajeti hiyo inatakiwa kulenga kwenye vipaumbele maalumu ambavyo
vinagusa maisha ya wananchi ya kila siku na sio ya kulenga watu wenye
vipato vya juu tu

  Kwa upande wake mmoja wa wananchi  hao aliyejitambulisha kwa jina La Enjo John alisema kuwa kwa sasa maisha ya
watanzania hususani wenye kipato cha chini wanashindwa kumudu milo
mitatu kwa siku kutokana na baadhi ya bidhaa kuuzwa kwa bei ya juu
sana kitu ambacho kinachangia kuongeza kiwango cha umaskini na lishe
duni kwenye baadhi ya familia.

alitolea mfano wa bidhaa za sukari, mchele, mafuta, nguo ambapo
kutokana na kipato ambacho wanapata baadhi ya watanzania kinasababisha
wakose mahitaji hayo ambayo ni muhimu kwa siku.

“bajeti hiyo inatakiwa itoe vipaumbele kwenye chakula kodi zisizo na
maana ziondolewe kabisa chakula kiwe na uhakika na kama itakuwa hivyo
watu wengi watapata fursa ya kuwa na afya njema na kisha kulitumika
taifa letu”aliongeza Emanulel Peter

  Aliongeza kuwa bajeti ya serikali
inatakiwa kutoa vipaumbele kwenye sekta ya elimu,afya,pamoja na
uwekezaji wa ndani

Alisema   Kwa upande wa  sekta ya afya kunatakiwa kuwe na huduma bora
ambapo huduma hizo ni pamoja na wingi wa vituo vya afya, lakini pia
hata dawa ,nyumba za watumishi, pamoja na huduma ya mama na mtoto kwa
kuwa kwa maeneo ya vijijini wanawake wengi wanafariki wakati wakiwa
wanajifungua.

Kwa upande wa wanawake wa jiji la Arusha walisema kuwa bajeti
inatakiwa ikidhi mahitaji muhimu hususani ya elimu kwani asilimia
kubwa ya wanawake wanabeba majukumu ya kusomesha familia zao.

Mmoja wa wanawake hao,ambaye ni mwalimu wa shule ya sekondari Nasholi
  Aggness Limo alisema kuwa bajeti inayokuja ilenge kuboresha
mazingira ya walimu ikiwepo nyumba za kuishi ,kuboreshewa maslahi
pamoja na wanafunzi kuongezewa vitabu vya kiada na ziada kwani
vimekuwa ni changamoto kubwa sana mashuleni.

Nae mmoja wa   askari usalama alisema kuwa ni vema bajeti inayokuja
ikatoa vipaumbele kwa maaskari kuboroshewa mishahara ,kuongezewa
vitendea kazi vya kisasa na kujengewa nyumba za kuishi kwani baadhi ya
maaskari wanaishi nyumba ambazo hazina hadhi na wao.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post