MAofisa
wa SABMiller na wafanyakazi wa TBL wakiwa katika picha ya pamoja wakati
wa maadhimisho hayo ambapo pia TBL Group ilitunukiwa tuzo kwa kendeleza
kilimo cha zao la Shahiri nchini
Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha akihutubia wananchi
Mkuu wa Uendelezaji Kilimo cha Shahiri wa SABMiller
kanda ya Afrika Thinus Van Schoor akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya
Wakulima wa Shahiri
.Naibu Waziri wa Kilimo,Chakula na Maendeleo ya
Uvuvi,William Ole Nasha (kushoto) akimpongeza mkulima wa Shayiri kutoka Kijiji
cha Lendikinya wilaya ya Monduli,Masiaya Oloshuda aliyeshinda kwenye bahati
nasibu ya kupata vifaa vya usalama shambani
Wakulima wa zao la Shahiri kanda ya Kaskazini
mwa Tanzania wanaoshirikiana na kampuni ya TBL Group wameadhimisha siku yao wilayani
Karatu ambapo mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Naibu Waziri wa
Kilimo,Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha wakiwemo wadau wao kutoka
SABMiller,na makampuni mengine yanayouza
madawa na pembejeo za kilimo.
Wakulima waliweza kufanya maonyesho
mbalimbali ya kazi zao pia walielezea
mafanikio walioweza kuyapata kutokana na kilimo cha zao la Shahiri