Na Woinde Shizza,Arusha
MKOA
wa Arusha, umefanikiwa kupata madawati 22, 756 na bado una upungufu wa
madawati 2577 ili kukamilisha madawati 24,373 ambayo yanahitajika kwa
ajili ya shule za msingi za mkoa ambazo hazina madawati.
Hayo
yameelezwa na Katibu tawala wa mkoa wa Arusha, Richard Kwitega,
wakati wa kuwatunuku vyeti vya madaraja matatu tofauti ya wadau
waliochangia madawati kwa kutambua mchango wao katika kuboresha elimu
kwenye hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa..
Kwitega,
ambae ametunuku vyeti hivyo kwa niaba ya mkuu wa mkoa, Daud Felix
Ntibenda, amesema mkoa huo una jumla ya wanafunzi 285,844 kuanzi darasa
la kwanza hadi la saba mwaka 2016, na mahitaji ya Madawati ni 119,765,
yaliyokuwepo ni 95,394 .
Amewapongezafanyaiashara kwa moyo wao huo na lengo ni kuhakikisha ifikapo julai mosi hakuna mwanafunzi anae kaa chini .
Akikabidhi
hati hizo kulingana na mchango uliotolewa na kampuni,Kwitega, amesema
serikali inatambua na kuthamini moyo wao wa uzalendo wa kujitolea sehemu
ya mapato yao kuchangia madawati kwenye shule za msingi mkoa wa Arusha.
Vyeti
hivyo ni vya Fedha, Shaba na Dhahabu, ambapo waliochangia madawati 1
hadi 10,ambao ni 20,wametunukiwa hati a Fedha, waliochangia madawati 11
hadi 19 ,ambao ni 15 wametunukiwa hati za shaba na waliochangia madawati
kuanzia 101, na kuendelea ambao ni 5 wametunukiwa hati za dhahabu.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo mkuu wa mkoa wa Arusha,Daud Felix Ntibenda,
amewaomba wafanyabiashara hao kuendelea kuchangia madawati 2577
yanayohitajika ili kukamilisha mahitaji ya mkoa ambayo ni 24,337.
Amesema
katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa ameunda timu ya wataalamu
kwendalaya zote na shule zote ili kujiridhisha kama madawati
yanatosheleza au bado kuna upungufu.
Ntibenda,
amesema Juni 18 ,2016, anaanzisha zoezi la kupita kwenye maduka makubwa
na viwanda kwa ajili ya kukusanya madawati yaliyopungua.
Amesema
wapo baadhi ya wafanya biashara wakubwa hawajaitikia wito huo hivyo
kutumia utaratibu huo wa kuwapitia wataweza kuchangia madawati.
Ntibenda,
amesema Julai mosi mwaka huu anaenda kuwsilisha taarifa ya madawati kwa
Rais, hivyo hayuko tayari kufukuzwa vkazi kwa kushindwa kufikia malengo
ya madawati katika mkoa wakati wapo watu wenye uwezo hawajatoa
michango yao.
Ameongeza
kuwa ameshakutana na watumishi wa serikali waliopo chini ya ofisi ya
Katibu tawala wa mkoa ili nao kila mmoja achangie dawati moja kwa kuwa
nao wana watoto waliopo shuleni na tayari amechangia madawati 692.